Rais Samia akishiriki Sherehe ya Kufunga Kozi ya Maafisa na Wakaguzi wa Jeshi la Polisi Juni 9, 2025
Hii si Afya kabisa kwa Usalama wa Umma.
Jeshi la Polisi limepoteza uhalali wote kabisa wa kuweza kuendelea kuwa Jeshi la Serikali katika nchi yoyote ile kutokana na Jeshi hilo kujihusisha na Vitendo viovu vya uhalifu mbaya, vitendo hivi viovu vinakwenda kinyume kabisa na Malengo ya awali ya kuanzishwa kwa Jeshi hilo.
Suluhisho pekee lililobaki kwa Sasa ni kulivunja Jeshi lote kabisa sambamba na kuanzisha Jeshi la Polisi lingine jipya kabisa, chini ya Sheria Mpya pamoja na miongozo mingine mipya itakayosimamia Jeshi hilo.
Kimsingi, Jeshi la Polisi lililopo hivi Sasa hapa nchini lina sura mbaya Sana kwa Umma, Wananchi karibia wote kabisa waliopo katika nchi hii tayari walishapoteza imani nalo tangu zamani.
Kwa Sasa, kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha kati ya Mapolisi na Majambazi/Watekaji.
Siku hizi Vituo vya Polisi siyo Vituo vya Usalama tena kama ilivyokuwa miaka ya zamani, Bali vimegeuka na kuwa Kambi za Kifo na Mateso kwa Raia wema! Siku hizi pia ukiitwa kwenda kwenye Kituo Cha Polisi chochote kile ni sawa sawa na Nusu ya Kukiona Kifo, ukiitika wito wenyewe ni sawa sawa na Kukubali Kifo!
Ukisikia ndugu yako amekamatwa na Polisi au ameitwa aende akaripoti katika Kituo Cha Polisi, basi unapaswa Ujiandae vizuri Kisaikolojia na uwe tayari kwa kupokea taarifa za msiba na kwenda kuchukua maiti ya ndugu yako!