Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mawaziri wateule Ikulu jijini Dar es Salaam leo tarehe 03 Oktoba, 2022
Nawapongeza kwa walio hapa. Mhe. Angela siyo mgeni kwenye kazi hii, umejifunza mengi ukiwa nje. Nimeona uje unisaidie. TAMISEMI ni ileile uliyoiacha.
Katika viapo tunaapa kulinda na kutetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kile kiapo ni chenu. Ni katiba ya JMT, Muungano wenye pande mbili, na mtatumika sehemu zote sawa kwa jinsi katiba ilivyogawa majukumu.
Mnapaswa kujua mipaka kwamba nchi hii ina Mamlaka, na mamlaka uliyowekewa ina mipaka yake, unapotaka kuvuka lazima upate ruhusa ya Mamlaka ya Juu. Sasa kujua mipaka yenu wakati mnafanya kazi, kwenda juu lakini pia kushuka chini, lazima mjue.
Tunzeni siri, aidha imesemwa kwenye Baraza la Mapinduzi, aidha umeitwa ukaelezwa, hiyo ni siri. Unapotaka kuisema, au kuifanyia kazi ujue jinsi ya kuitumia hiyo siri. Linaloamuriwa na Serikali ni lako, lazima ulibebe na ulifanyie kazi kwa misingi ile uliyoelekezwa. Huwezi kusema nilielekezwa hivi, mimi sikutaka hivi lakini imebidi nifanye hivi kwa sababu nimeelekezwa, huwezi kujitoa.
Mnapaswa kuheshimu Katiba, kujua mipaka na kutunza siri.