Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akizindua mradi wa maji Kigamboni na kugawa mitambo ya Kuchimbia visima, Leo Novemba 11, 2022
=====
Mradi wa maji wa Kigamboni umezinduliwa rasmi na Rais Samia, Rais amejafungua maji na yanatoka kwa wingi.
Rais amekata utepe na kukabidhi magari ya kuchimbia visima na mabwawa na kukabidhi funguo. Magari hayo yatatumika kuchimbia visima vijijini na mijini, pia ameagiza magari hayo yakatunzwe.
Hotuba ya Rais Samia Suluhu
Awali ya yote nijielekeze Kumshukuru Mungu kwa kutukunanisha hapa leo, kama mnavyoelewa wiki iliyopita ajali ya ndege ilitokea hivyo naomba tusimame kwa dk moja tuwaombee ndugu zetu.
Nitumie nafasi hii kutoa shukrani zangu kwa Waziri wa maji kwa kunialika kwenye shughuli hii, ya kukabidhi magari kuchimbia visima vya maji, kukabidhi ardhi kwa mkandarasi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda na Kufungua mradi wa Maji Kigamboni.
Nawaachia kazi DAWASA kuhakikisha Kigamboni inapata maji kwa asilimia 100 kwani imekuwa ikitoa maji Dar ila yenyewe haipati maji, Dar ilitikiswa na ukosefu wa maji kutokana na mabadiliko ya tania ya nchi, na hii ni kutokana na watu kuchepusha maji, kupeleka mifugo na shughuli nyingine za kiuchumi.
Waziri wa mifugo naomba mkae muangalie njia ya kufanya mifugo isizagae ovyo, na hii ni nchi nzima, Picha niyooneshwa hapa ni ng'ombe karibu 5000 na ng'ombe 1 anakunyw alita karibu 45 kwa siku kwa ng'ombe 5000 ni lita ngapi watakunywa na waachie maji ya kuchujwa kuleta kwa wananchi, lakini endeleeni kutoa elimu na hic=zo picha pelekeni TBC zionekane kwa jamii ili waone uharibifu unaofanywa.
Katika miaka miwili hii wanangu wa idara ya maji umeifanya kazi nzuri sana, niwaombe ongezeni juhudi kwani kumpatia mwanandamu maji ni sadaka, ongezeni juhudi na wanasema mcheza kwao hutunzwa hivyo huko mbele tutakuja kuwatupia jicho la rehema, na serikali itaendelea kutoa fedha.
Kila mmoja ahakikishe kulinda miundombinu na vifaa vyite vilivyotolewa kwani vinanunuliwa kwa gharam kubwa, na visipotunzwa vitaharibika haraka. Tambue mitambo hii imegharibu bilioni 35 fedha ambazo zingeweza kufanya mambo mengine hivyo mtunze.
Mitambo hii ikatumike kama ilivyokusudiwa kwani inauwezo wa kutambua eneo lenye maji na si kuchimba kisima halafu maji hakuna, mkimbicha kisima maji hakuna sitawavumilia waliohusika nataka wawajibishane wao kwa wao kabla ya kufika kwangu.
Pamoja na kugawa mitambo lakini leo tumezindua mradi wamaji ni matumaini yangu shida ya maji itakwenda kupungua Dar, tunatambua mradi huu ni wa kupunguza makali tu lakini suluhisho la kudumu ni ujenzi wa bwawa la Kidunda na mkataba umesainiwa na linakwenda kuanza kujengwa. Likimaliza kujengwa na kujaa tuna uhakika hakutakuwa na shida ya Maji Dar, nitoe rai kwa makandarasi kukamilisha kazi hii kwa viwango vilivyokusudiwa na kwa wakati.
Pamoja na juhudi za serikali kuhahakisha wanapata huduma ya kuvuka Kigamboni kama tulivyoanza kuwashirikisha sekata binafsi tutaendelea kuwashirikisha sekta binafsi, pamoja na kuagiza kivuko kipya kijengwe kikijengwa tutawakabidhi sekta binafsi wakiendeshe halafu tunaelewana huko kwenye mikataba.
Jambo lingine ni daraja la Kigamboni, kuna tozo na watu wanaomba ziondoke, haziwezo kuondoka kwa kuwa ni mkopo na watu inabidi wazoee kuna miradi migni ya aina hii itakuja ili tuendele. Watu wanatolea mfano daraja la Tanzanite, lile ni fedha ya serikali kwa asilimia 100 ila hii ya kulipia ni uzoefu wa mwanzo ile bure inabidi iondoke tuwe na miradi mikubwa madaraja makubwa ila yakiwa ya mikopo wa kulipa mikopo hiyo ni sisi waanchi na inabidi tuzoee kulipa. Hatutaweza kuondoa tozo labda tuone namna ya kuipunguza.