Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Rais Wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
Amekoshwa ,kufurahishwa na Kuguswa sana na mapokezi mazito na ya heshima aliyoyapata na kupewa kutoka kwa maelfu kwa maelfu ya wananchi wa Manyara hususani Hanang ambao wamefurika na kumiminika kama mchanga wa Baharini kwa ajili ya kuweza kumpokea na kumsikiliza.
Ambapo Rais na Mama yetu Mpendwa kwa unyenyekevu mkubwa kabisa kama ilivyo kawaida yake ya kujishusha kwa Wananchi ameahidi kuwatumikia kwa uaminifu , unyenyekevu na weledi wa hali ya juu sana katika kuwaletea maendeleo.
Amesema ya kuwa mapokezi makubwa ambayo amekuwa akiyapata ni ishara ya kukubalika na imani kubwa waliyonayo wananchi kwa chama cha Mapinduzi yaani CCM. Na kuahidi kuendelea na kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi wote kwa kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo itakayogusa maisha ya kila mmoja Pasipo kumuacha mtu yeyote yule nyuma.
Ikumbukwe ya kuwa Mama na Rais wetu na Mgombea wetu kupitia CCM yupo katika kampeni kwa mikoa ya kanda ya kaskazini. Ambapo tangia kuanza kwa kampeni hizo za Urais na kupita katika mikoa mbalimbali Bara na visiwani amekuwa akipata mapokezi makubwa na ya heshima kubwa sana kutoka kwa watanzania.
Ambapo kila mkutano unavunja rekodi ya mkutano uliotangulia. imefikia hatua ni kama watu wanashindana kuhudhuria katika mikutano yake . Maana watu wanafurika utafikiri Tanzania nzima wamekutanika eneo moja tu alipo Rais Samia. Kinachoendelea kwa sasa ni Mahaba na upendo mkubwa sana wa watanzania wanaompatia na kumuonyesha Rais Wetu.
Kwa hakika Mama ni mtu na kiongozi wa watu anayependwa ,kukubalika na kuaminika sana machoni na mioyoni Mwa Watanzania. Hii ni kwa kuwa ndani ya muda mfupi wa uongozi wake ameonyesha uwezo mkubwa sana wa kiuongozi,Kugusa maisha ya watu,kuleta maendeleo kila eneo,kujenga miradi ya maendeleo kila sehemu , kuinua uchumi na kujenga uchumi jumuishi au Shirikishi,kuwawezesha watu kutimiza ndoto zao pamoja na kujenga Tanzania yenye kuleta matumaini kwa kila mmoja mwenye kufanya kazi na kujituma kwa bidii.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.