..Yes, we can do that.
..Sasa huyo ' Consultant ' atakuwa Mkenya?
..Hiyo siyo aibu kweli?
Mkuu 'JokaKuu', pamoja na kukubali aibu hiyo..., mimi nadhani tunalo tatizo kubwa zaidi ya lugha pekee.
Hili nakumbuka tulishalijadili sana hapa kati yetu.
Hadi hapo serikali itakapokubali kuimarisha elimu yetu kwa ujumla, tatizo halitakuwa lugha tu, lakini uimara wa elimu yenyewe ya wahitimu wetu.
Tumeona mara nyingi sana katika vyuo mbalimbali huko majuu, hususani Uingereza na Marekani, wanafunzi wachina, waIran, WaIraq, na kutoka mataifa mengi mbalimbali wakiingia vyuo bila kujua lugha ya kufundishiwa masomo katika vyuo hivyo (Kiingereza); hawa wanapewa miezi mitatu (siku 90) kujifunza lugha, na wanapomaliza muda huo wanaendelea na masomo bila shida yoyote!
Sasa maajabu ni kwa mTanzania, anayejifunza lugha hiyo sijui tokea darasa la ngapi siku hizi, mtu anamaliza chuo kikuu, na hata anachukua PhD, katika lugha ile ile; bado mtu huyu anakuwa na matatizo hata ya kujieleza tu hata kama lafudhi haikunyooka?