Pamoja na mapungufu yake kama binadamu sote tulivyo, lakini tukubali kwa kauli moja kwamba Dk. Magufuli hakuwa binadamu wa kawaida kimaono, kiutendaji kazi na ufatiliaji wa karibu.
Baadhi ya watu wanajaribu kumsema mambo mengi mabaya Magufuli walwatu,lakini nawakumbusha kwa mara nyingine tena kwamba hakuna Rais yeyote Tanzania pamoja na barani Afrika ambaye aliwahi kuwa mbunifu na muona mbali kama Magufuli - miradi yote mikubwa ya kimkakati inayo endelea hapa Tanzania mwanzilishi wake si mwingine bali Magufuli - ndani ya utawala wake mfupi wa miaka mitano amebuni na kutekeleza miradi mikubwa mikubwa ambayo kwa akili za kawaida uwezi kui-comprehend hata kidogo - halafu watu wenye akili za ajabu wana beza beza miradi na maendeleo yaliyo letwa na mzalendo wa kweli wa Taifa hili.
Wengi wanao mchukulia Magufuli for a ride wanashindwa mpaka na Umoja wa mataifa ambao ulimuenzi wakati alipo aga Duniani kwa kutambuwa sana mchango wake wa kuwaletea maendele binadamu wenzake specifically Tanzanians - kila mara Magufuli alikuwa anatukumbusha kwamba tutakuja kumkubuka - na kweli!! Bottom line ni kwamba: tunapo mlahumu the late Dk. Magufuli tujifunze kubakiza hakiba ya maneno.
Kitu kingine ambacho huwa akina ukweli wowote ni hiki cha kudai eti ukoo wa Magufuli hauna asili ya Tanzania - huu ni uzushi husiokuwa na kichwa wala miguu - ukweli wa mambo ni kwamba kabila la Magufuli ni Mzinza, sio Msukuma mama yake ndio Msukuma na Magufuli alikuwa fluent kwenye lugha ya Kisukuma kutokana na mama yake kuwa Msukuma, kabila la Kizinza has nothing in common na kabila la Kisukuma, mila za Kizinza zinarandana zaidi na mila za Kihaya, hata lugha ya Kizinza haina tofauti sana na lugha ya Kihaya.
Hayati Magufuli ni mmoja wa watanzania ambao wanajitambua na yeye alikuwa ni mtu aliejitambua.
Hii ni sifa moja kubwa sana ya binadamu, kujitambua.
Hayati Magufuli alijitambua na hata wengine kama mimi Richard najitambua.
Watanzania waafrika wengi na hata baadhi ya wazungu waliweza kuona hilo kuwa hayati Magufuli alijitambua na aliweka alama ya bara la Afrika kwenye koti lake.
Sasa baadhi ya wazungu na waafrika wengine hawapendi kuona waafrika wenzao wanajitambua maana wanahisi hapatashikika.
Kama hayati Magufuli aliweza kutikisa kila mahali na pakatikisika na akaja nchini bwana mkubwa wa uchimbaji madini kutoka Canada, basi alikuwa ni yeye na hatatokea Magufuli mwingine tena ndo imetoka hiyo.
Lakini bara la Afrika bado lina waafrika na watanzania wengi ambao bado hawajajitambua na ikifika siku wanajitambua itakuwa ni siku ya kiama na tutakuwa tumechelewa maana yeye alikwishasema tumecheleweshwa mno.
Ushuhuda ni madudu ambayo yameanza kurudi baada ya kuondoka kwake duniani, mara TRA kuna mitambo imeharibika, mara TANESCO mfumo wa LUKU umeingiliwa, mara majambazi yamerudi na mara bandarini kuna figisu zimerudi hii yote ni kuonyesha kuwa watanzania bado hawajaweza kujitambua.
Hapo awali , tulisikia mara Kitalu C kilianza kuingiliwa mpaka pale mama Samia alipoamuru ulinzi uimarishwe.
Pia tumesikia wizara ya fedha watu wamesimamishwa kazi kwa ubadhilifu wa fedha na hiyio ni wizara ya FEDHA yaani hazina ya nchi!
Hivyo, kwanza watanzania waweze kujitambua kuwa wao ni nani na wapo Tanzania kwa kusudio la Mungu ambae amewapa rasilimali na uwezo mkubwa wa kumiliki rasilimali hizo hivyo wahitaji usimamizi.
Kinachohitajika ni kujitambua, kisha kuhakikisha twazisimamia rasilimali hizo na kuzigeuza kuwa utajiri kiasi cha kumsaidia kila mtanzania aliezaliwa Tanzania na yule alie na vinasaba vya utanzania kwa elimu bora, makazi bora na maisha bora.