Bulamba
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 13,741
- 13,049
Je hali ilikuwaje wakati wa shujaa?Watu kama Dangote wanahitaji serikali zenye watu wenye akili sana na ujuzi wa namna wafanyabiashara wakubwa walivyo. I bet if we have that brain NOW
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je hali ilikuwaje wakati wa shujaa?Watu kama Dangote wanahitaji serikali zenye watu wenye akili sana na ujuzi wa namna wafanyabiashara wakubwa walivyo. I bet if we have that brain NOW
Shida kubwa ya Dangote ni mtu anaeamini in monopoly. Sehemu zote anapowekeza huwa ana bad reputation ya ku corrupt viongozi wa kisiasa ili kuua competition nahisi ndio maana hawakuwezana na mwendazake.
Mkuu, washindani wake wenye viwanda vya saruji hapa nchini wataungana na kumpiga vita vya chini chini Dangote kama walivyo fanya mwaka juzi - kuna mambo ya wa ajabu nchi hii yenye lengo la kukwamisha wawekezaji wenye uwezo mkubwa kimtaji - haya mambo yakusema eti Taifa linaruhusu biashara uria ni hiyo ni danganya toto - waulizeni WavietNam walipo kuja na pendekezo la kushusha gharama za ununuzi wa bundle za data na voice - kampuni kubwa za simu nchini ziliwatisha tisha WavietNam wa watu mpaka wakaingia laini - sikuona TCRA wala inaingilia kati ku-support juhudi za HaloTel kuwapatia wananchi unafuu wa gharama za mawasiliano mpaka tunashindwa na nchi kama Rwanda.Huyu mjukuu wa aliko Dan tata afanye mchakato cement irudi elf 10 Ili wanyonge tuachane na nyumba za nyasi
,,Kila kitu kimebadilika na hakikika wawekezaji wataludi,,tusubiri tuone
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu kutokea Nigeria Alhaji Aliko Dangote
Mazungumzo hayo muhimu yalifanyika leo Mei 24, 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam
Alhaji Dangote ni mfanyabiashara mkubwa duniani aliyewekeza nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kiwanda cha kuzalisha Saruji Mkoani Mtwara
Alhaji Dangote amemshukuru sana Rais Samia kws kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea
Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na alwaagiza Mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote
Taarifa zaidi kutolewa na Mamlaka husika
Kazi Iendelee
Pengine hufahamu effect ya monopoly. Once akiwa ndie pekee anae endesha biashara ya cement tegemea kuwa ata control bei. Mlaji siku zote ana fadikia kwenye soko lenye ushindani. Mwogope mtu mwenye imani ya monopoly kama ukoma.Kama Monopoly ambayo anapenda Dangote anatuuzia cement bei poa kama ile ya 10,000,(vunja bei) safi kabisa...sasa sie wananchi huyo ndo afadhali atuokoe kuliko maviwanda hayo mengine,yanayotukomoa kwa bei za cement za juu kila uchwao.... kazi iendelee yaVunja bei....
Mwendazake hayati rais John Pombe Joseph Magufuli, mwenyewe alilalamikia watu wake serikalini kwa kukwamisha malengo ya Dangote kule kusini:
Awamu zote Tanzania imekuwa na wawekezaji na matokeo yamekuwa hasi/chaya kuligana na msimamo/maono ya Rais aliyeko madarakani pale Serikali:-Sasa figisu za nini kama kodi anawalipa? muacheni afanye kazi kwa amani, hii mikutano ya aina hii ndio inafungua njia kwa wawekezaji wengine kuwa na amani ya kuja kuwekeza Tanzania.
Safi,Awamu zote Tanzania imekuwa na wawekezaji na matokeo yamekuwa hasi/chaya kuligana na msimamo/maono ya Rais aliyeko madarakani pale Serikali:-
[emoji830]︎ Awamu ya Kwanza - Ujamaa: utaifishaji na umiliki wa njia kuu za uchumi, palipo stahili ushirikiano na wawekezaji;
[emoji830]︎ Awamu ya Pili - Rukhsa: kufanya chochote/lolote lakini hapukuwa na uwekezaji wa maana zaidi ya kuibua Misheni Town;
[emoji830]︎ Awamu ya Tatu - Utawala Bora: ubinafsishaji wa njia kuu za uchumi, wawekezaji wakabadili km viwanda kuwa maghala ya bidhaa zao kutoka nje;
[emoji830]︎ Awamu ya Nne - Ari mpya na Kasi mpya: Tanzania yageuzwa shamba la bibi. Tunashuhudia uwekezaji kwenye sekta ya anasa km mahoteli, majumba ya starehe, na "shopping malls";
[emoji830]︎ Awamu ya Tano - Hapa Kazi tu: ujenzi wa miundo mbinu na kuboresha huduma za jamii kwa fedha za ndani. Kufanikisha hilo mianya ya kukwepa kodi inazibwa na baadhi ya wafanya biashara wanazifunga na kuzihamishia nje ya nchi; na
☆ Awamu ya Sita - Kazi inaendelea: Diplomasia ya uchumi kushawishi wawekezaji kutoka nje mradi hawaifanyi Tanzania shamba la bibi tena.
KABISA mkuu. Haowezekani Mtanzania asili uwe na Roho Ile. Yaani hata Wa Tanzania walowezi humu nchi ni wengi tu na walikuwa au wana vyeo lakini si kwa hali Ile. Na Wasukuma nijuavyo si wa tabia is Ile kabisa. Kuna wakati iliubuliwa miaka kadhaa iliyopita kuhusu asili yake? Babu yake migrated to Tz and his father was born in Tanzania but he claimed that his father acquired Tz Citizenship??? No wonderUkichunguza sana, Mwendazake wala hakuwa na asili ya Tanzania.
Wanaosema msukuma nakataa kabisa, hana hata dalili ya usukuma ndani yake!
MONDAY MAY 24 2021
Dar es Salaam, Tanzania
Aliko Dangote impressed by dramatic change in Tanzania's business environment
Dar-es-Salaam, Tanzania
Video courtesy of Global TV online
![]()
President Samia meets Nigerian businessman Aliko Dangote at State House, Dar es Salaam.
Aliko Dangote, Africa's richest man, has praised Tanzania's President Samia Suluhu Hassan, saying that the business environment in the country had changed "dramatically" under her leadership.
Read more : Source : Dangote impressed by dramatic change in Tanzania's business environment
Umenena vema kabisa. Sera za Uwekezaji inatakiwa iwe ni mipango ya Kimkakati ya Ki-Taifa tena ya muda mrefu. Sera ya Uwekezaji haipaswi kubadilishwa pale Kiongozi mmoja anapoondoka na kubalisha uongozi wa Kitaifa. Ndio maana Uwekezaji Tanzania umekuwa ukisuasua mno kwa kile Wawekezajia wanacho kilalamikia kuwa "luck of seriousness and vision" ya viongozi wa Tanzania kwenye masuala mazima ya Uwekezaji mkubwa na wa kimkakakati.Tutengeneze sera za kudumu kwenye uwekezaji siyo akija mwingine ana haribu na kukimbiza wawekezaji
Majukumu ya Rais ni nini hapo?Haya ndiyo majukumu ya Rais sasa
Rais ndiye balozi/mwanadiplomasia namba 1 wa nchi, Moja ya jukumu lake kubwa ni kuunganisha nchi na jumuiya ya kimataifa. Siyo kila kitu unamtuma FM or VP, uzito wa kuwepo wewe kama Rais ni mkubwa kuliko kutuma watuMajukumu ya Rais ni nini hapo?
Hebu nambie Samia na Dangote wamekutana kufanya nini?
Dangote amealikwa Ikulu kuja kufanya nini?
Jibu swali.Rais ndiye balozi/mwanadiplomasia namba 1 wa nchi, Moja ya jukumu lake kubwa ni kuunganisha nchi na jumuiya ya kimataifa. Siyo kila kitu unamtuma FM or VP, uzito wa kuwepo wewe kama Rais ni mkubwa kuliko kutuma watu
Haya ndiyo majukumu ya Rais sasa, siyo kutafuta cheap popularity kwa watu wenye upeo finyu (Machinga, bodaboda, mamantilie na wauza nyanya wa Dumila), matokeo yake unaenda hadi kuzindua vyoo na kuwaambia watu waache mavi yao nyumbani. Hongera Mother
Mkuu Babati kwa kuwa una chuki na uongozi wa CCM badala ya kuwa mchambuzi, kwa maslahi mapana ya Taifa, hujapenda kusoma na/au kufuatilia utekelezaji wa Ilani zake za Uchaguzi ambazo kimsingi ni mikakati ya kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa (Development Vision 2025).Tutengeneze sera za kudumu kwenye uwekezaji siyo akija mwingine ana haribu na kukimbiza wawekezaji
Ba ndio sababu ya mkuu wa mkoa alipangiwa kazi nyingineMadereva wake wameajiriwa kama contractors badala ya kupewa full time employment, hilo linawakosesha haki zao za kisheria nyingi ikiwemo uhakika wa kazi zao, kuingizwa kwenye pension schemes, kwenda likizo ya malipo, sick pay na faida wanazopewa wafanyakazi wenzao; bila ya kusahau kupoteza PAYE za TRA.
Hayo ndio mambo ya kumkubusha na yeye. Juzi tu madereva wa Dangote walikuwa kwenye mgomo kisa kuchukuliwa kama vibarua wakati watu wanafanya kazi sehemu moja zaidi ya miaka miwili, hakuna madereva wenye mkataba wa kudumu na kampuni; kuna middleman anaewapa ajira na kuwapunja kwa kuwakata kilicho chao, bila ya ulazima.
Wafanyabiashara sio kuja kuomba mazingira mazuri tu, bali na wao waweke mazingira mazuri kwa waajiriwa, sakata lote la mgomo limeenda karibu week nzima Mhagama kama alikuwa aoni vile na nina uhakika wale madereva madai yao ya msingi ayajatatuliwa.
Ni kweli kabisa mkuu kama hili la kutuletea wasiojulikana na kuanza kuteka watu ovyo naona ulilitamani sanaAhsante sana Bagamoyo,
Kweli teknologia haiongopi, ndio hiki nimekizungumzia, na hapo nimesikia hata huo mpango wa kujenga kiwanda cha mbolea ulikuwa toka hicho kipingi cha Magufuli.
wamlaum kwa mambo mengine lakini haki yake apewa,
kwangu mimi Magufuli amefanya mambo ambayo watanzania tuliyalilia muda mrefu.