Madereva wake wameajiriwa kama contractors badala ya kupewa full time employment, hilo linawakosesha haki zao za kisheria nyingi ikiwemo uhakika wa kazi zao, kuingizwa kwenye pension schemes, kwenda likizo ya malipo, sick pay na faida wanazopewa wafanyakazi wenzao; bila ya kusahau kupoteza PAYE za TRA.
Hayo ndio mambo ya kumkubusha na yeye. Juzi tu madereva wa Dangote walikuwa kwenye mgomo kisa kuchukuliwa kama vibarua wakati watu wanafanya kazi sehemu moja zaidi ya miaka miwili, hakuna madereva wenye mkataba wa kudumu na kampuni; kuna middleman anaewapa ajira na kuwapunja kwa kuwakata kilicho chao, bila ya ulazima.
Wafanyabiashara sio kuja kuomba mazingira mazuri tu, bali na wao waweke mazingira mazuri kwa waajiriwa, sakata lote la mgomo limeenda karibu week nzima Mhagama kama alikuwa aoni vile na nina uhakika wale madereva madai yao ya msingi ayajatatuliwa.