Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Nakubaliana na wewe partly serikali izibane kampuni zote zinazochukua contacts za mashirika na kuajiri watu wengine kufanya hizo kazi. Kampuni husika lazima wafuate sheria za kazi na kuhakikisha agency workers wa muda wanapata entitlement zote.Ukitaka manufaa ya cement iwe Tshs. 10,000 kwa mfuko lazima kazi zingine zifanyike na macontractors waliopewa kazi kama za usafirishaji, payroll iwe sub contracted kwa watu wengine n.k ili menejimenti ya Dangote Cement ijikite katika core duties uzalishaji na kuhakikisha mashine mitambo ya viwanda inakwenda sawa.
Masuala mengi ya human resources, maduka ya cement waachiwe wengine wafanye. Huu ndiyo mtindo wa kisasa wa ku - run operesheni za viwanda vikubwa ktk dunia hii ya mapinduzi ya viwanda ya nne.
Hutakiwi kufuatilia sijui likizo, off ya kuumwa, kutazama watoto, kufiwa / msiba, mishahara ya madereva na wafanyakazi wengine wasio wataalamu wa cementi au wa uendeshaji kiwanda haya yote unawapatia ma contractor waumize vichwa masuala yasiyohusisha uzalishaji.
Hapa inatakiwa serikali izibane kampuni hizi zinazofanya kazi ya u contract wa madereva , payroll n.k kuwapa wafanyakazi wake wote wanaopelekwa kufanya kazi za Dangote Cement mishahara, stahili, likizo, mikataba na marupurupu, posho kufuatana na sheria za kazi za Tanzania.
Kuilaumu kampuni ya Dangote Cement ambayo haihusiki na uajiri wa hawa madereva na wafanyakazi wengine wa agency ni kupoteza muda. Serikali iwabane ma contractor waliobeba majukumu ya ajira za wafanyakazi hawa.
Huo nduo utakuwa mwarobaini, utakaofanya watu kama kina Dangote waajiri badala ya kutoa contracts zisizo na lazima ili kukwepa majukumu ya kisheria.
Utakuta kwa sasa Dangote wanalipa mishahara tu kwa contractors ivyo vigezo vikiwekwa na contractor nao wataongeza charge, will that be worth it to Dangote maana hao watu wanahitaji for full time and for many years too.
Je wakiwa nje ya control zao watakuwa motivated kutokana na uhusiano wao na huyo contractor wakati Dangote wanalipa kila kitu, hayo sasa ndio yatabaki maswali kwa Dangote kama waajiri au waendelee na mfumo wa kutoa contracts kwa third parties.
Lakini haki za wafanyakazi lazima ziheshemiwe wawe wanaajiri kupitia contractor au moja kwa moja.