Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

I agree
 
Afadhali,, cement itashuka bei, maana walimfanyia figisu mwanzoni, wakati ule cement ya dangote imeshamili mtaani, tulinunua mfuko wa saruji hadi Tsh 10,000 kutoka 15000.

Dikteta alimfanyia figisu za kutisha.
Hilo jina dikteta utalitapika siku...waulize Libya kinachowakuta sasa hv.... nao walisema Gaddafi ni dikteta
 
Hilo jina dikteta utalitapika siku...waulize Libya kinachowakuta sasa hv.... nao walisema Gaddafi ni dikteta
Haitatokea kumkumbuka magufuli, ila atakumbukwa ni dikteta wa kwanza kutokea Tanzania,

Na kwa upande wa ccm washajifunza, nimeambiwa kwenye katiba ya Ccm wanataka kuweka kipengele cha waomba kuteuliwa wawe wanapimwa afya ya akili
 
Kwenye barakoa ndipo sijaelewa, wakiwasilisha wawili wamevaa barakoa, kwenye kundi la kupinga picha hawajavaa barakoa.
Only in Africa.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Haitatokea kumkumbuka magufuli, ila atakumbukwa ni dikteta wa kwanza kutokea Tanzania,

Na kwa upande wa ccm washajifunza, nimeambiwa kwenye katiba ya Ccm wanataka kuweka kipengele cha waomba kuteuliwa wawe wanapimwa afya ya akili
Shida za watu kama wewe ni ukabila tu ndo unakusumbua. Nakumbuka uchangiaji wako, umekuwa ni wa mlengo wa kikabila tu! Subili siku urais utakapoangukia kwenu.
 
Haitatokea kumkumbuka magufuli, ila atakumbukwa ni dikteta wa kwanza kutokea Tanzania,

Na kwa upande wa ccm washajifunza, nimeambiwa kwenye katiba ya Ccm wanataka kuweka kipengele cha waomba kuteuliwa wawe wanapimwa afya ya akili
Haitatokea kumkumbuka Magufuli....kwako sio kwangu na wengine wote waliomuelewa...

Km kuwabana watu wasitafune hii nchi ni ugonjwa wa akili basi CCM watupe vichaa maana ndio tunawahitaji..

CCM wapime raisi ambae anauchungu wa hii nchi na anatambua km hii nchi ni ya wakulima na wafanyakazi ambao ni maskini...na infact ingependeza zaidi wangetupatia kiongozi mwenye background ya ukulima...mabraza meni waliosoma mjini baadae wakapelekwa nje na baba zao hatuwataki maana hao hawaijui nchi hawajui umaskini tulionao vijijini...watakaa kuwaza wazungu/wawekezaji ndio watatukumboa...wengine tumesomeshwa na mifugo mpaka sasa tunapumua kwa mifugo huyo mzungu tunamsikia radioni tu..

Nasikia tuna madini ila mpaka leo mkulima trekta ni anasa...anakuja kiongozi anatuambia tunaibiwa tujenge ukuta tulinde madini yetu anaitwa dikteta..hv tumelogwa
 

Kwa nyongeza: tuna viwanda vikubwa vya Saruji km Twiga, Tanga na Mbeya. Nasubiri kama navyo vitalindwa kwa nguvu ile ile au vitaachwa vimezwe na Dangote!
 
Shida za watu kama wewe ni ukabila tu ndo unakusumbua. Nakumbuka uchangiaji wako, umekuwa ni wa mlengo wa kikabila tu! Subili siku urais utakapoangukia kwenu.
Tanzania ya leo inao wapuuzi wengi sana haswa mitandaoni wanaowasakama sana wasukuma, kama vile ni watu fulani wachache sana.

Tushukuru Mungu msingi wetu ni umoja, vinginevyo wasukuma kama wangekuwa ni watu wajeuri siku nyingi sana wangeshaiharibu hii amani tunayojivunia.

Ni hulka mbovu sana kuwasakama wasukuma kama vile ni watu fulani wasio na hisia zozote. Kuna watu wanaiombea nchi hii kila wakati ndio maana inaweza kuvipita vipindi vingi vya hatari.
 

Nakubaliana na wewe kwa kuwa mikakati ya Serikali ya utekelezaji wa Ilani ya Chama chake, km Kilimo kwanza, usimamizi wake umekuwa ya kudodora. Ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo (Development Vision) 2025, ni dhahiri tunahitaji Kiongozi jasiri, anayethubutu kufanya maamuzi magumu, na mwenye Utashi wa Kisiasa.

Kwangu mimi, ukiacha Baba wa Taifa ambaye pamoja na mengi aliyofanikisha, alijenga utaifa kupitia Siasa ya Ujamaa na kujitegemea (Azimio la Arusha), ni Hayati Magufuli. Hayati Magufuli pamoja na mapungufu makubwa katika kukuza demokrasia, alifanya na kusimamia maamuzi magumu ya kujenga Taifa linalojitegemea. Wakati Hayati Mkapa yeye alijikita kwenye Utawala bora.

Kuhusu swali lako mama hata halijulikani anasimamia nini? jibu yawezekana ikawa ni kubomoa misingi ya "Taifa la kujitegemea" iliyowekwa na mtangulizi wake kama ambavyo wafuasi wa Baba wa Taifa na Hayati Mkapa walivyobomoa misingi yao (Azimio la Arusha na Utawala Bora).
 
Investment inahitaj mazingira wezeshi na support kutoka serikali husika, huez ku investment kwa kutegemea figusu.
Ni kweli uwekezaji unahitaji mazingira rafiki ya kijumla siyo ya kibaguzi. Mazingira ya uwekezaji kwa mwananchi ni magumu sana kuanzia kupata ardhi, leseni hadi mikopo ya mitaji.

Kwa hali inavyoonekana na kuelekea, wananchi wataendelea kuwa wajiriwa kwenye nchi yao yenye fursa nyingi za uwekezaji katika Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda, Madini, na Utalii. Hata sekta ya Sanaa na Mziki ambayo imevamiwa na vijana wengi, mazingira ya uwekezaji nayo si rafiki kwa wawekezaji wa ndani.
 
Waziri wa Mambo ya Nje ya Saudia Arabia Mwana wa mfalme Mhe. Faisal Bin Farhan Al Saud azungumza leo Ikulu Dar es Salaam Tanzania kuhusu uwekezaji na mahusiano baina ya nchi hizi mbili:



25 May 2021
Dar - es Salaam, Tanzania

Tanzanian President Samia Suluhu Hassan receives Saudi Arabia’s Foreign Minister Prince Faisal bin Farhan.


Source : michuzi tv
 
Wewe umeajiri wangapi unadhani ni rais hivyo wakati kipindi cha mwendazake kufanya biashara? wengi walikimbia na hata Dangote alisema ni vigumu kufanya biashara Tanzania
 
Unaota ww unadhan huyu ni ngichiro kama ww
Hivi Kwa nini hawa wafanya biashara wakubwa huwa wanakaa kudekadeka saana!!!

Huyu jamaa anaongoza Kwa kudeka, haishiwi kulalama kama litoto Fulani hivi, Mo, na Bakhlesa, sjawahi kuona wakideka hivyo
 
Je, mwekezaji anaweza kwenda kufanya figisu kwenye nchi ya kigeni? Si ataswaga fasta!
 
Sawa
 
Unaota ww unadhan huyu ni ngichiro kama ww
Mkuu, nataka kukuuliza, unadhani Lugha ya kuudhi kiasi hiki imewahi kukusaidia chochote...! Je, unadhani unaowaambia maneno hayo, bila kujali mchango wao hawakutoa tusi wala Neno la kuudhi, halafu wewe unakuja kuwatusi maneno ya kuudhi, kwani wao hawafahamu kutokwa maneno hayo?

Mkuu, jiheshimu basi ili uheshimiwe...!
 
Hayati Magufuli ni mmoja wa watanzania ambao wanajitambua na yeye alikuwa ni mtu aliejitambua.

Hii ni sifa moja kubwa sana ya binadamu, kujitambua.

Hayati Magufuli alijitambua na hata wengine kama mimi Richard najitambua.

Watanzania waafrika wengi na hata baadhi ya wazungu waliweza kuona hilo kuwa hayati Magufuli alijitambua na aliweka alama ya bara la Afrika kwenye koti lake.

Sasa baadhi ya wazungu na waafrika wengine hawapendi kuona waafrika wenzao wanajitambua maana wanahisi hapatashikika.

Kama hayati Magufuli aliweza kutikisa kila mahali na pakatikisika na akaja nchini bwana mkubwa wa uchimbaji madini kutoka Canada, basi alikuwa ni yeye na hatatokea Magufuli mwingine tena ndo imetoka hiyo.

Lakini bara la Afrika bado lina waafrika na watanzania wengi ambao bado hawajajitambua na ikifika siku wanajitambua itakuwa ni siku ya kiama na tutakuwa tumechelewa maana yeye alikwishasema tumecheleweshwa mno.

Ushuhuda ni madudu ambayo yameanza kurudi baada ya kuondoka kwake duniani, mara TRA kuna mitambo imeharibika, mara TANESCO mfumo wa LUKU umeingiliwa, mara majambazi yamerudi na mara bandarini kuna figisu zimerudi hii yote ni kuonyesha kuwa watanzania bado hawajaweza kujitambua.

Hapo awali , tulisikia mara Kitalu C kilianza kuingiliwa mpaka pale mama Samia alipoamuru ulinzi uimarishwe.

Pia tumesikia wizara ya fedha watu wamesimamishwa kazi kwa ubadhilifu wa fedha na hiyio ni wizara ya FEDHA yaani hazina ya nchi!

Hivyo, kwanza watanzania waweze kujitambua kuwa wao ni nani na wapo Tanzania kwa kusudio la Mungu ambae amewapa rasilimali na uwezo mkubwa wa kumiliki rasilimali hizo hivyo wahitaji usimamizi.

Kinachohitajika ni kujitambua, kisha kuhakikisha twazisimamia rasilimali hizo na kuzigeuza kuwa utajiri kiasi cha kumsaidia kila mtanzania aliezaliwa Tanzania na yule alie na vinasaba vya utanzania kwa elimu bora, makazi bora na maisha bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…