Rais Samia alijifunza nini akiwa Makamu M/Kiti wa Bunge la Katiba 2014?

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Ki ukweli nimesikiliza hotuba ya Mh Rais Samia leo kwenye mkutano na wadau wa Demokrasia nimekosa jibu la moja kwa moja kuwa licha ya kuwa Rais Samia aliwahi kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge la Katiba mwaka 2014 bado haikulitumia kama funzo bunge lile!

Maswali ninayo jiuliza leo hii!

1. Rais Samia anaamini kuwa kwakuwa wananchi kwa 50% hawakuwa na uelewa juu katiba ndiyo walisababisha mchakato wa Katiba kukwama?

2. Rais Samia hakujua nani au wakinani walivuruga mchakato wa Katiba mwaka 2014?

3. Rais Samia hakujifunza kuwa mara baada ya kuandika katiba pendekezwa itahitajika Elimu kwa wananchi wanakubali Katiba pendekezwa na wanaoipinga ili waipigie kura wananchi?

4. Rais Samia aliona Report za tume ya katiba ikisema kuwa wananchi hawana uelewa wowote juu ya katiba?

5. Rais hakumbuki kama kuhodhi kwa mchakato wa katiba kwa CCM (JAKAYA) Ndiko kulipelekea mchakato wa katiba mpya mwaka 2014 kukwama?

6. Rais Samia hajui kama Katiba si mali yake na wala hana mamlaka nayo?

Mbona kama Rais amekuwa kama mgeni na mtu ambae hajawahi kubisa sio kushiriki tu au ata kusikia mabadiliko ya Katiba?

 
Kuna mambo yanatafakarisha sana.Madaraka hasa ya juu humuondolea mtu akili zake za awali na kumpatia nyingine kwa ajili ya anapokuwa kwa wakati huo?🤔
 
Kiongozi wa mpito anapokiuka maelekezo ya wenyenchi!!
 
Badili ya kujiuliza wewe umejifunza nini unauliza mama Samia kajifunza nini! Unashangaza.

Mama Samia mbona kaelezea vizuri kabisa, kuwa muda ni mdogo mpaka uchaguzi ujao.

Hivi unashindwa kuelewa kuwa huu ni mwaka wa uchaguzi na mwakani ni mwaka wa uchaguzi? Na watendaji ni hao hao.

Mbona vitu vipo wazi kabisa.
 
CCM HAITAKI KATIBA MPYA SUALA LA ELIMU NI VIJISABABU TU TENA VISIVYO NA MASHIKO
 
Kwa hotuba ile ya jana ni kama inasikitisha zaidi
 
[emoji867]
 
Nilitaka kushangaa,Samia asemwe na usicomment kumtetea
 
Nilitaka kushangaa,Samia asemwe na usicomment kumtetea
Hivi hapa anasemwa mama Samia?

Mdomo kazi yake kusema, mradi tusiutumie huohuo kulia chakula na huohuo kutukana, kuna midomo mingine ya matusi.

Sawa sawa?
 
Kumbe duniani watu wengi ni wanafiki.
Usiwaamini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…