Ndugu Samia Suluhu alipitishwa mwaka 2022 na MM Taifa kuwa Mwenyekiti Taifa wa CCM baada ya nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na kifo cha JPM. Lakini kuhusiana na suala la urais wake hakuna kikao chochote kile kimewahi kumpa idhini ya kugombea nafasi hii.
Si kikao cha KK, Halmashauri Kuu ya Taifa wala MM Taifa wa chama chake kimewahi kufanya hivyo. Aliyepewa ridhaa hiyo na vikao hivi ni JPM. Sijui katiba ya CCM inasemaje kuhusiana na hili, lakini mimi naona ni kinyume hata na mila na utamaduni wao.
Mwaka 2015 zilitolewa fomu nyingi, mwaka 2020 ilitolewa fomu moja ili kumpisha JPM amalizie awamu yake. Sasa 2025 zinapaswa zitolewe nyingine nyingi ili makada wapimane ubavu kwa ajili ya kumpata yule anayekubalika zaidi. Acheni uoga, kama Samia anakubalika sana ndani ya chama chake, basi si aache taratibu zichukue mkondo wake!