Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Binafsi, naamini Rais Samia alipochukua madaraka, alikuwa na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya mifumo ya kiutawala, yaani kutengeneza nchi ambayo watu wake wataongozwa kwa haki, kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa maoni, na kisha kujenga uchumi wenye misingi ya haki. Hii ndiyo ilikuwa sababu yake ya kuja na falsafa ya 4Rs.
Katika kuingia kwenye uhalisia, maana yake Rais Samia alikuwa anaingia kwenye kazi ngumu sana ya kuwabadilisha watu ambao wanajua kabisa kuwa uwepo wao katila nafasi walizopo ni kutokana na dhuluma dhidi ya umma wa Watanzania. Hii ilikuwa ni kuanzisha vita dhidi mifumo dhalimu ya ndani ya Serikali na ndani ya chama chake, mifumo iloyoota mizizi na kupata nguvu kwa miaka mingi.
Kubadili mifumo, tena inayoshikiliwa kidhalimu na watu wenye nguvu ndani ya chama na Serikali siyo jambo jepesi, ili kufanikiwa:
1) Rais Samia alihitaji kuwa na watu wenye nguvu na jasiri kweli kweli ambao wangeweza kusimamia utekelezaji. Bahati mbaya Rais Samia aliwakosa watu hao na akalazimika kuwatumia wale wale wafuasi wa mifumo dhalimu ambao aliwakuta. Hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.
2) Ili afanikiwe, alistahili kutengeneza msingi imara wa kuungwa mkono na umma katika kuleta mabadiliko. Na hapo alistahili kutafuta uungwaji mkono kutoka makundi yote, kuanzia ndani ya chama chake, vyama vya upinzani, taasisi mbalimbali, na umma kwa ujumla, na hilo lingeganyika kwa kuuelimisha umma ambao kwa muda mrefu umefungiwa katika ujinga. Ilitakiwa kuweka wazi ubaya na ubovu wa mifumo iliyopo, na kureleza wazi tunataka kujenga Taifa la watu gani. Ili kufanya hayo kwa mafanikio, alistahili kuondoka kuwa Rais wa CCM, na kuwa Rais wa Watanzania wote, na hiyo ilistahili idhihirike wazi kwa kauli na vitendo. Kwenye hili Rais Samia hakufanikiwa sana kwa sababu mara kadhaa alivishambulia vyama vya upinzani na kuipamba CCM, ambayo kimsingi ndicho baba wa huu udhalimu wote kwani ndicho kilichotengeneza hii mifumo dhalimu ya utawala Inayolisumbua na kuligandamiza Taifa.
3) Ili Rais asimamie haya mabadiliko, hakustahili kutekwa fikra zake kupitia hoja za kushindwa kwenye uchaguzi kama ambavyo wale wadhalimu wamekuwa wakimtishia. Hivyo ili kumwondolea hofu, hata kwa kupitia mifumo isiyo rasmi, angefanywa kuwa Rais wa mpito, yaani kwa kudhihirisha dhamira yake njema, kwa kilaalu wamekuwa wakifanya. njema, Rais Samia angeungwa mkono na vyama vyote vyenye dhamira njema, kwenye uchaguzi , vikijua kuwa baada ya kipimdi cha mpito, utafuata uchaguzi wa ushindani wenye mazingira safi na huu uchafu tulio nao sasa.
Kwa hali ilivyo sasa, kwa Rais Samia kukosa mikakati na mbimu sahihi, waumini wa mifumo dhalimu ndani ya CCM na Serikali, wameweza kumzidi nguvu na kumfanya na yeye aonekana kuwa ni sehemu yao. Sasa tunashuhudia falsafa yake ya 4Rs ikichomwa moto na watekaji watu, ikiuawa na wasiotaka katiba bora, na kichanwachanwa na wasiotaka tume bora ya uchaguzi. Utengamano alioufikiria kuujenga umefutika, na uovu umepata nguvu mpya ya ajabu kiasi cha wananchi wengi kuona kuwa 4R ni falsafa ya hadas ambayo haikuwa na dhamira ya kweli.
Mtihani mkubwa kwa Samia upo mwaka huu na mwaka kesho, ambapo wadhalimu watautumia uchaguzi kummaliza na kumchafua kabisa Rais Samia mbele ya umma. Na mbele ya uso wa jamii ya kimataifa.
Kwa sasa watu dhalimu ndani ya CCM na Serikali wanafurahia ushindi wao dhidi ya falsafa ya 4Rs.