McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Mgombea Urais kupitia CCM Samia Suluhu Hassan amesema kwa Jimbo la Kigoma Mjini Wagombea Ubunge wa mwaka huu wa CCM Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Babalevo na Zitto Zubeir Kabwe wa Chama cha ACT Wazalendo wote ni wanae na wananchi ndio watakaoamua nani awaongoze.
Dkt. Samia ameyasema hayo Septemba 14, 2025 wakati wa Mkutano wake wa kampeni Kigoma Mjini, akilazimika kueleza hayo kutokana na ombi la Baba Levo aliyemuomba Dkt. Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kumtaja mgombea anayemuunga mkono kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
"Sina utani, nitampiga mtu saa tano asubuhi kwasababu ninayeshindana nayi mtu dhaifu sana, ni maarufu (gangwea) kwenye mitandao lakini ukimleta huku chini ni biskuti. Ni kama ameshahamia CCM maana leo alikuwa anasambaza vipeperushi vya Oktoba tunatiki akiwa amemuweka Mama na yeye pale chini, nakuomba Mama ni muda wa kumuambia ukweli unamsapoti nani hapa Kigoma Mjini." Amesema Baba Levo.
Katika majibu yake pamoja na mengine, Dkt. Samia amemjibu akisema
"Nataka kuwaambia wote ni watoto wangu kwasababu hata yule mwingine katoa vibao vya kijani na njano vinasema mpe Mama Samia, Ubunge nipe mimi sasa si unajua kwenye nyumba watoto wakiwa wawili watatu wanavutana sio ndio? Lakini wote ni wanangu."