Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo ya jumla ya uongozi ya mwanamke kinara jijini Mwanza huku akishukuru na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa masilahi ya Taifa.
Tuzo hiyo ilitolewa usiku Aprili 5, 2025 mkoani Mwanza na taasisi ya Mwanamke kinara iliyoandaa tuzo za wanawake waliofanya vizuri katika sekta mbalimbali kanda ya ziwa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Akizungumza kwa njia ya simu baada ya kupokelewa tuzo hiyo na Kadogosa, Rais Samia alisema anawashukuru waandaaji kwa kuona mchango wake na ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya wananchi na masilahi ya Taifa.
"Ninashukuru sana kwa tuzo kutoka kwa wanawake wa mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi...Ninawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa, mimi kama mama mmenipa utulivu ndio maana nimeweza kuyafanya niliyoyafanya.
"Tumeweza kuboresha sekta ya maji, umeme na barabara , ahadi yangu ni kuendelea kuwatumikia wananchi na Taifa kwa kadri Mungu atakavyonijalia," amesema Rais Samia.
Pia, Soma