MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 65
- 81
Utendaji wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia serikali ya awamu ya sita anayoiongoza umekua sumu kali kwa upinzani nchini kwani umewanyima wapinzani agenda za kusimama nazo kwenye majukwaa ya kisiasa kumnanga na kumshambulia. Zaidi wamebaki kufanya siasa za kibaguzi kwa kushambulia asili yake (Mzanzibar).
Hizi ndio agenda ambazo utekelezaji wake umeunyima pumzi upinzani
1. Amefanikisha kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini ambapo Chini ya Uongozi wake Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazolinda uhuru wa vyombo vya habari Afrika Mashariki . Pia katika upimaji wa uhuru wa habari duniani kaitoa Tanzania toka nafasi ya 143 mwaka 2023 hadi nafasi ya 97 mwaka 2024 kwa mujibu wa utafiti uliotolewa na Reporters Without Borders (RFS) Mei 3,2024.
Aidha ameendelea kulinda uhuru na haki ya kujieleza ya kila raia bila kuvunja sheria.
2. Ameruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa iliyokuwa imesimama kwa takribani miaka 6. Hii imetoa fursa kwa vyama vya siasa kuhamasisha umma, kutoa elimu ya uraia, kunadi sera zao na kuikosoa serikali kwa hoja.
3. Ameruhusu kufanyika kwa maandamano ya kisiasa bila kizuizi na kutaka jeshi la polisi litoe ulinzi kila yanapofanyika. Chama Cha Demokrasia na Mandeleo ni mnufaika mkubwa wa uamuzi huu.
4. Uwazi wa serikali kuhusu masuala ya mikopo na taarifa za ukaguzi za mkaguzi na mthibiti wa hesabu za serikali (CAG) kwa umma zimeonesha kupungua sana kwa upigaji wa fedha za umma hali inayopelekea fedha nyingi kwenda kwenye miradi ya maendeleo.
5. Ametoa kipaumbele kwenye maendeleo ya watu kwa kutekeleza miradi inayowagusa wananchi moja kwa moja kama vile ukamilishaji wa miradi ya kimkakati (Mradi wa uzalishaji umeme Bwawa la Nyerer - JNHPP, Ujenzi wa SGR, Ujenzi wa bomba la Mafuta, ujenzi wa bandari ya uvuvi Kilwa nk), miundombinu ya umwagiliaji, usafiri na usafirishaji (kwa maana ya barabara, reli, viwanja vya ndege, shirika la ndege, shirika la meli, bandari nk), miradi ya uboreshaji na uimarishaji wa miundombinu ya elimu, afya, maji safi, nishati nk
Kwa haya machache yameuweka upinzani rehani. Siasa ni maendeleo, Twende na Samia!
#TwendeNaSamia2025
#SamiaTena2025
#HakunaKilichosimama
#KaziIendelee