Rais Samia alivyowasili nchini India kwa ziara ya Kikazi ya siku 4

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasili jijini New Delhi, India leo tarehe 08 Oktoba, 2023 kwa ajili ya kuanza ziara ya kitaifa ya siku nne nchini humo.

Mapokezi rasmi ya Rais Samia yatafanyika tarehe 09 Oktoba, 2023 ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa India, Droupadi Murmu kwa pamoja na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi.

Ziara ya Rais Samia nchini India ni mwendelezo wa ushirikiano na uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili ambapo sekta muhimu nchini kama Afya, teknolojia, kilimo, uchumi wa buluu, biashara, uwekezaji, maji na elimu zinatarajiwa kuwa kipaumbele cha majadiliano wakati wa ziara hii.
Your browser is not able to display this video.
 
Kuna uzi tayari uwe unasoma wengine kabla ya kuanzisha uzi
 
[emoji2956][emoji2956][emoji2956]
 
Uhusiano haswa ....

Soko letu la MBAAZI....

#UDUMU USHIRIKIANO WA TANZANIA NA INDIA[emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…