Rais Samia aliweka wazi kuhusu ongezeko la mshahara, 23.3% ni kwa kima cha chini tu. Watumishi acheni lawama mara moja

Hizi hasira sio bure kuna kitu hakipo sawa kwenye medula

Ww ndio Una hasira kwa kuleta Uzi WA kutukana watu as if they are outcast in this country! Kwa mtu anaejitambua, anaheshimu na mwenye akili zilizotulia, huheshimu mawazo, hisia na utu wa Binadamu mwenzake. Na kama umeelimika vizuri, Una heshimu kazi za Binadamu wenzako. Na sio kushambulia Kada flani eti kwa sababu ww uko Kada nyingine.

Nakuhakikishia, ww Una frustration!
 
Mimi naheshimu kila mtu, Ila kwenye ukweli nitasema hata kama ni ukweli mchungu
 
Akili ninazo kiasi zinatosha kuendesha maisha yangu.

Nimeuliza salary slip ziko wapi maana katika mfumo hazijawekwa wewe umeziona wapi?

Kama umeziona jikoni kabla hazijatoka nijibu tu sio ugomvi mkuu
Anachanganya Payroll na Salary Slip.....
 
Mimi naheshimu kila mtu, Ila kwenye ukweli nitasema hata kama ni ukweli mchungu
Huheshimu Binadamu wenzako na kazi zao ww. Una dharau sana, na hii itakugharimu Sana hata kama sio wewe. Ila kizazi chako pia, hakuna mtu aliyemaliza vyema, au kizazi chake kikawa salama kwa kudharau watu ndugu! nakuhakikishia, wewe una dharau sana kwa watu ambao kwa hisia yako, na uono wako hafifu unawaona ni wa Chini kipato, maisha, au mazingira. Tena kama wewe ni mtumishi na Una cheo, ni mnyanyasaji Sana, na kama ni mtumishi au mfanyakazi wa kawaida huna relationship nzuri na wenzako! Nina uhakika, kwa dini yangu. Aise! Wewe ni mnyama sana tena mwenye dharau sana.
 
Mimi ndio Countrywide, ni Kama Msumari wa moto, kadri unavyoukalia ndio utavyokua unaumia. Hii JF mmeifanya kuwa kama darasa, kila mara mnakuja na mambo ya ajabuajabu tu ni lazima tuwachane na kuwaweka sawa mpaka mbadilike
 
Maslahi duni
Unaona sasa, walikuja kugundua hawapo sehemu sahihi wakaamua kuacha.

Mimi hoja yangu ipo kwa hawa ambao wapo. Mtu aliyekua anatenda dhambi akaamua kuokoka unamhubiria nini? Tunahubiri kwa walio kwenye dhambi
 
Hapo kusema kwa kazi gani unazofanya umeonesha una chuki na walimu, kwani ungeishia tu kusema uchumi haukidhi ungepungukiwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…