Rais Samia aliweka wazi kuhusu ongezeko la mshahara, 23.3% ni kwa kima cha chini tu. Watumishi acheni lawama mara moja

Rais Samia aliweka wazi kuhusu ongezeko la mshahara, 23.3% ni kwa kima cha chini tu. Watumishi acheni lawama mara moja

inategemea na kazi gani anafanya, muda anaotumia katika hiyo kazi, mahali anapofanyia, aina ya teknolojia inayotumika na kazi hiyo inahitaji uwekezaji kiasi gani katika viwango vya elimu, na hatari ya kufanya hiyo kazi ni kwa kiasi gani. Suala siyo tu kulinganisha kiasi cha malipo anayopokea.
Short and clear, Ukiona pesa ni ndogo acha kazi
 
Unacho na una upande kabisa. Hakuna mtu akaichukia CHADEMA na asiwe na Chama na hakuna mtu aichukie CCM na asipende chama fulani.
Ilipo HAKI nami nipo hapo.

CCM ikizingua naitandika, CDM ikizingua vile vile. Wakitenda vzr napongeza.

CCM Ina hazina kubwa ya viongozi waadilifu wengi tu, hawana Idadi. Ina wavamizi na wahuni wengi pia.

CDM Ina viongozi wazuri na wahuni pia wapo.

Muhimu ni Maendeleo ya Watanzania wote. TUTAFIKA TU.
 
Acha serikali ijitetee kwa matendo yake na sisi tujitetetee kwa wajibu....serikali sio ya kuionea huruma ..Ningekuwa nimeongezewa kwa miaka sita ya mwendapole Ningekuwa nanusa 1.7m...
 
Baada ya kuzunguka huko na huku hatimaye wamejua ongezeko la mshahara, lawama zimeanza na wengine kuanza kumshambulia raisi. Hii haikubaliki hata kidogo.

Raisi aliweka wazi ongezeko la mshahara kwa 23.3% ni wale wa kima Cha chini, Ila kutokujua kusoma na kuelewa kwa watumishi kukafanya ionekane ni kwa watu wote.

Ni kama kuna watu walijiandaa kutoa lawama kwa raisi wetu ikiwa taarifa ilisema wazi kabisa kuwa ni kima cha chini. Hata hivyo tukirudi kwenye uhalisia kwa uchumi ulivyoyumba duniani na Tanzania tukiwemo, unawezaje kuhitaji ongezeko la 23.3%?? Kwa kazi gani hasa unazofanya?

Watumishi wengi ni walimu, zaidi ya nusu(300000+) na hawa ndio waliokuwa mstari wa mbele kupotosha ongezeko ili mwisho wa siku ionekane serikali iliongopa. Shida ni nini kwenye hii kada ya ualimu? Ufahamu mdogo?

Narudia tena acheni lawama kwa Raisi mara moja, na pia mshukuru hata kwa hiko kidogo mlichopata.
Yaani unaona kuwa walimu ndio watumishi wa umma tu
 
Ni kwamba akili hauna?

Akili ninazo kiasi zinatosha kuendesha maisha yangu.

Nimeuliza salary slip ziko wapi maana katika mfumo hazijawekwa wewe umeziona wapi?

Kama umeziona jikoni kabla hazijatoka nijibu tu sio ugomvi mkuu
 
Akili ninazo kiasi zinatosha kuendesha maisha yangu.

Nimeuliza salary slip ziko wapi maana katika mfumo hazijawekwa wewe umeziona wapi?

Kama umeziona jikoni kabla hazijatoka nijibu tu sio ugomvi mkuu
Upo idara gani?
 
Kama mmepungukiwa akili nitawabeza tu
Halafu kuwa mwalimu sio big deal wala sio laana. Watu wengi ni walimu na wanaendesha maisha yao vizuri pengine kukuzidi wewe uliyepungukiwa na akili. Waziri wako mkuu walimtoa kwenye vikorido vya hapo tamisemi akiwa kama nani? Samia mwenyewe unaye muinamishia kichwa na kuacha makalio nyuma mmoja wa wazazi wake alikuwa mwalimu.

WALIMU CHAPENI KAZI ACHANENI NA PSYCHOPATHS KAMA HAWA
 
Unaposema shida ni walimu kuwa na uelewa mdogo wewe ulifundishwa na Nani ili uwe na uelewa mkubwa? Hivi kauli "Serikali imeridhia ongezeko la mishahara kuwa 23.3% kwa watumishi ikiwemo kima Cha chini kunahitaji PHD kujua maana yake? Acha dharau ndg, kuwa mwalimu usidhani ndo watu hawana uelewa wa mambo ndo maana Mwl aliitoa nchi hii chini ya ukoloni, ni kada ipi nyingine ilidhubutu kuzungumzia uhuru wa nchi tofauti na kulamba miguu ya wazungu?
 
Kesho Kuna watu watapata aibu ya karne, uliposemwa kuongeza wakadai haiwezekani nchi haina uwezo, sasa wanaanza fitina za kipumbavu kabisa
 
Sawa kwahiyo sema wazi kabisa sasa kwamba
Baada ya kuzunguka huko na huku hatimaye wamejua ongezeko la mshahara, lawama zimeanza na wengine kuanza kumshambulia raisi. Hii haikubaliki hata kidogo.

Raisi aliweka wazi ongezeko la mshahara kwa 23.3% ni wale wa kima Cha chini, Ila kutokujua kusoma na kuelewa kwa watumishi kukafanya ionekane ni kwa watu wote.

Ni kama kuna watu walijiandaa kutoa lawama kwa raisi wetu ikiwa taarifa ilisema wazi kabisa kuwa ni kima cha chini. Hata hivyo tukirudi kwenye uhalisia kwa uchumi ulivyoyumba duniani na Tanzania tukiwemo, unawezaje kuhitaji ongezeko la 23.3%?? Kwa kazi gani hasa unazofanya?

Watumishi wengi ni walimu, zaidi ya nusu(300000+) na hawa ndio waliokuwa mstari wa mbele kupotosha ongezeko ili mwisho wa siku ionekane serikali iliongopa. Shida ni nini kwenye hii kada ya ualimu? Ufahamu mdogo?

Narudia tena acheni lawama kwa Raisi mara moja, na pia mshukuru hata kwa hiko kidogo mlichopata.
"WALIMU HAWANA AKILI"
 
Back
Top Bottom