SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Hivi majuzi kulikuwa na mjadala mkubwa uliohusiana na uamuzi wa Simba kuvaa jezi za "Visit Tanzania" na wakati huo huo Yanga kukataa kuvaa nembo hiyo badala yake wakaingia mkataba na kampuni ya Haier.
Huu mjadala ulijikita zaidi katika kuuliza ni maslahi gani Simba wanapata kwa kutangaza nchi. Wengine tulisisitiza faida hizi zinaweza kuja mbele siyo tu kwa nchi lakini pia kwa club.
Siku ya leo, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika wizara mbili ya Michezo na ile ya Utalii. Waziri Mohammed Mchengerwa na Katibu wake Dr. Hassan Abbas waliokuwa Wizara ya Michezo wamehamishiwa Wizara ya Utalii. Wakati huo huo Dr. Pindi Chana aliyekuwa Wizara ya Utalii amehamishiwa Wizara ya Michezo.
Ni nadra sana kukuta mabadiliko ya namna hii ambapo Waziri na Katibu wake wanahamishwa kwa pamoja kwenda wizara moja na wale wanaochukua nafasi zao kuja wizara wanayotoka. Ingawa sipendi siasa naona huu unaweza kuwa uamuzi wa kimkakati wenye lengo la kujenga mbinu na mashirikiano ya karibu kati ya wizara hizi mbili.
Utalii wa Michezo una nafasi kubwa katika kukuza utalii nchini. Tusiishie tu katika soka bali tuangalie pia michezo mingine, na ikiwezekana tubuni michezo mipya inayoweza kukuza utalii.
Nadhani serikali katika mipango yake ikumbuke juhudi za Simba katika kukuza utalii. Wale ambao waliweka biashara mbele badala ya utaifa waachwe wakafie mbali.
Ninapatikana kwa ushauri pale nitakapohitajika 🤣😂🤣