Rais Samia ameamua kuwatolea uvivu Jeshi la Polisi na kuyaanika hadharani maovu yao!

Kuyaanika NI jambo la kawaida kwani sote tunajua ila je hatua gani za kuchukua angesem hata alivunje jeshi kwa muda Kisha vituoni wakae wanajeshi ingekuwa safi
Watu wengi tunaamini jeshi la wananchi ni safi, lakini uaminifu wao ni kwasababu hawakutani mara kwa mara na raia, hivyo hawapati mianya mingi ya kupiga pesa kwa raia.
 
Mfano, kati ya aliyoongea kuhusu kubambikia watu kesi, na kuwaonea raia, haya yametokea wakati wa utawala wake, na mojawapo wa wahusika, Kingai, amempandisha cheo na kumfanya awe DCI, sasa nitayaamini vipi maneno ya Rais?!
Wanasiasa sio watu wa kuaminika kabisa kwa kweli!
 
Kuyaanika madudu ili wakayatazame huko , haitoshi!!
Tunahitaji ofisa wa ngazi za juu, ashitakiwe kwa makosa yanayofanywa dhahiri na baadhi ya maafisa wa polisi.
Ndani ya Polisi kuna mtandao mbaya.
Kuna Ofisa alifanya ubambikaji wa kesi ya silaha mwaka 2012, akagundulika na kuwekwa kitimoto.
Ma god father w huyo ofisa, aliyekuw Wazo, wakamtorosha kwenda mikoani.
Baada ya muda akawa RPC wa Mkoa!

Rais Samia bila kuondoa mtandao wa uhalifu NDANI ya Polisi, itakuwa kazi kubwa kulipa discipline jeshi hili.
 
Kuanika uozo ni jambo moja na kusimamia mabadiliko ya kuondoa uozo no jambo lingine huu ni wakati wa kusimamia uozo uondoke sio kuuanika tu
Hiyo ni hatua moja, kuelekea huko tunakopania kwenda
 
Lakini mheshimiwa rais ametukosea sana kutuletea Kingai Kama DCI!.
 
Nikikumbuka tozo, naona gharama ya tozo ni kubwa kuliko rushwa( kwani sisi tunatoa tozo, ni faini ya kosa gani?).
Rushwa huwa wanaangalia uwezo wako na muktadha wa tukio. Lakini tozo hadi hela ya kununulia jeneza , sanda, hela ya matibabu, chakula, nauli inakatwa tozo.
 
PGO ni
 
Huyo kuimba ngonjera ni kawaida yake lakini utendaji ni zero kabisa
 
Ahaaa....yaani anaanika kitu kilichotandazwa juani kitambo. Yeye si mtu wa kuanika bali anatakiwa kuwa mchukua hatua, kuanika awaachie waandishi wa habari za kiuchunguzi.
 
Huyo kuimba ngonjera ni kawaida yake lakini utendaji ni zero kabisa
Lakini huoni tofauti Kati yake na yule Mwendazake, aliyekuwa akiwapongeza hao maaskari hadharani kwa hayo hayo madudu waliyokuwa wakiyafanya?
 
Vizurii

 
Hakuna jipya. Haya tunayajua kuliko hata yeye! Na tafadhali usisema ameanika hadharani wakati tayari yapo hadharani siku nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…