Rais Samia ameamua kuwatolea uvivu Jeshi la Polisi na kuyaanika hadharani maovu yao!

Lakini huoni tofauti Kati yake na yule Mwendazake, aliyekuwa akiwapongeza hao maaskari hadharani kwa hayo hayo madudu waliyokuwa wakiyafanya?
Tofauti gani? Angekuwa tofauti kama angechukuwa hatua za kulifumua jeshi la polisi na kuunda upya. Kusema haina tofauti yoyote na aliyekuwa anawasifia.
 
Lakini at least, ameonyesha kukerwa na tabia za hao maaskari, tofauti na yule wa awamu ya 5 ambaye amekuwa akiwasifu hadharani, kwa makosa hayo ambayo wamekuwa wakiyafanya!
Usiwaamini hawa watu kwani wanayoongea hadharani ni tofauti na wanayoyafanya nyuma ya pazia .
 
Lakini at least, ameonyesha kukerwa na tabia za hao maaskari, tofauti na yule wa awamu ya 5 ambaye amekuwa akiwasifu hadharani, kwa makosa hayo ambayo wamekuwa wakiyafanya!
Angalau mdomoni na machoni pa watu. Je matendo? huwezi kumchagua Kingai tukakuamini, watu wanaofikiri hawawezi kukuamini! Kingai?
 
Mbona hamkupiga kelele Kinana alivyotoa kauli hadharani trafiki wapunguzwe barabaran bila kufuata hiyo protokali? Huu ni unafiki unaletwa kwa sababu hizi

1) Ni Mzanzibari
2) Ni Muislam
3) Ni Jinsia Yake
 
Kila nikisoma kayanika kayaanika, kwaiyo bado kukauka?

Matendo mabaya ya polisi sio mapya, yanajulikana.
 
Lakini huoni tofauti Kati yake na yule Mwendazake, aliyekuwa akiwapongeza hao maaskari hadharani kwa hayo hayo madudu waliyokuwa wakiyafanya?
Action speaks louder than words
 
SSH anaweza kuwa na nia njema lakini bila kubadilisha/kurekebisha sheria bado amebadilisha kwa muda tu..
Polisi wanacheza kwenye udhaifu wa sheria ..
 
Hili lingevunjwa liundwe jipya. Ma graduates wako kibao mitaani. Inawezekana kuunda jeshi la kisomi kama Scotland Yard siyo hawa manungayembe yaliyo kubuhu kwa rushwa.
 
Lakini at least, ameonyesha kukerwa na tabia za hao maaskari, tofauti na yule wa awamu ya 5 ambaye amekuwa akiwasifu hadharani, kwa makosa hayo ambayo wamekuwa wakiyafanya!
Hajaanza kukerwa leo. Alipoingia tu madarakani alikemea tabia ya watu kubambikiwa kesi. Kwa yeye kuikemea tena kunaonyesha kuwa pengine kuna watu walikuwa hawajamuelewa.

Amandla....
 
Amiri jeshi anakerwa nini sasa hapa, yeye achukue hatua anayoona inafaa, sie wananzengo ndio tunaendelea kukerwa, polisi wanaiba mafuta hii ni jinai ni hatua tu ndio zichukuliwe hapa. Viongozi wao hawatakiwi kukerwa wao wanatakia kuchukua hatua sababu ya mamlaka waliyonayo.

Mtoto anachezea socket ya umeme muwambe kofii bara bara ili aone mzazi unakerwa ila akichezea moto ndio muache utamuunguza na hatarudia tena. Mama Polisi funga kweli kibwebwe katika idara ya hovyo nchi hii na inayohitaji overhaull ni polisi kama kweli Mama amekerwa basi achukue hatua kali kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…