Rais Samia amechangia millioni 200 Ujenzi wa kanisa Kuu la Christ Cathedral Church, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenan Laban Kihongosi, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Kuu la Christ Cathedral Church, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na kufanikisha kuchangishwa jumla ya Shilingi 418,445,000.

Harambee hiyo imefanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) Jijini Arusha, ikihudhuriwa na Mhashamu Baba Askofu Dkt. Stanley Hotay – Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), pamoja na viongozi wa dini, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Serikali na taasisi mbalimbali.

Katika hotuba yake, Mhe. Kihongosi amesisitiza umuhimu wa kudumisha umoja, upendo na mshikamano, hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Aidha, amepongeza mchango wa kanisa katika malezi ya watoto, jamii na kujenga maadili ya Taifa.

Ujenzi wa kanisa hilo unakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 3.8, na unatekelezwa kwa kuzingatia mpango kabambe wa Jiji la Arusha wa mwaka 2025 (Arusha Masterplan 2025). Ujenzi huo haujaathiri jengo la zamani lililojengwa mwaka 1932 ambalo litaendelea kuhifadhi historia ya nchi tangu kipindi cha ukoloni.

Harambee hiyo imeongozwa na maandiko kutoka Biblia, Ezra 10:4: "Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe, uwe na moyo mkuu ukaitende."

Misikumo ya siasa za kampeni. Na unaweza kukuta ni ahadi na sio fedha taslimu. Kenya nakumbuka kuna kanisa liligomea fedha za Ruto hapo.
 
Huyu mama bwana..wewe mama umekataliwa duniani na mbinguni embu tupishe bwana!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Kenan Laban Kihongosi, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Kuu la Christ Cathedral Church, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na kufanikisha kuchangishwa jumla ya Shilingi 418,445,000.

Harambee hiyo imefanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC) Jijini Arusha, ikihudhuriwa na Mhashamu Baba Askofu Dkt. Stanley Hotay – Askofu wa Dayosisi ya Mount Kilimanjaro na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), pamoja na viongozi wa dini, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Serikali na taasisi mbalimbali.

Katika hotuba yake, Mhe. Kihongosi amesisitiza umuhimu wa kudumisha umoja, upendo na mshikamano, hasa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Aidha, amepongeza mchango wa kanisa katika malezi ya watoto, jamii na kujenga maadili ya Taifa.

Ujenzi wa kanisa hilo unakadiriwa kugharimu Shilingi Bilioni 3.8, na unatekelezwa kwa kuzingatia mpango kabambe wa Jiji la Arusha wa mwaka 2025 (Arusha Masterplan 2025). Ujenzi huo haujaathiri jengo la zamani lililojengwa mwaka 1932 ambalo litaendelea kuhifadhi historia ya nchi tangu kipindi cha ukoloni.

Harambee hiyo imeongozwa na maandiko kutoka Biblia, Ezra 10:4: "Inuka; maana shughuli hii yakuhusu wewe; na sisi tu pamoja nawe, uwe na moyo mkuu ukaitende."

View attachment 3420538
Atatoa zote walizomhonga DP World kudadeki😂
 
Back
Top Bottom