kalacha mateo
Senior Member
- Sep 27, 2021
- 119
- 240
Leo Jumatatu ya tarehe 09/01/2023 wanafunzi wamefungua shule ikiwemo wanafunzi 1,073,941 walioanza kidato cha kwanza ambao wote walipangiwa shule hakuna mwanafunzi ambaye yuko nyumbani kusubiri chaguo la pili "Second Selections"
Ikumbuke tangu kuanza kwa utoaji wa elimu bila malipo nchini kumekua na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule za msingi na sekondari. Mkakati wa serikali ya Rais Samia Suluhu ulikua ni kuboresha mazingira ya elimu na kufuta chaguo la pili hivyo kuanzia mwaka 2021 ujenzi wa madarasa nchi nzima ulianza.
Mwaka 2021 serikali ya Rais Samia ilijenga madarasa 15,000 na Septemba mwaka 2022 ujenzi wa madarasa 8,000 ulianza na kufikia mwezi Desemba tayari yalikua yamekamilika kwa ajili ya kupokea wanafunzi Januari mwaka huu. Mpango huu ni endelevu kwani kupitia TAMISEMI wamefanya tathmini kubaini maeneo ambayo bado yana uhitaji wa Madarasa, walimu, vyoo, mabweni na maabara ili viweze kujengwa.
Serikali ya Rais Samia mbali na kuimarisha miundombinu bado imehakikisha elimu inatolewa bila malipo, mikopo inatolewa kwa wanafunzi wa vyuo pamoja na kuanza kuanzishwa kwa "Samia Scholarship".