Rais Samia ameitendea Haki Elimu nchini

Rais Samia ameitendea Haki Elimu nchini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Tangu kuingia madarakani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka 2021, shule za msingi mpya zaidi ya 468 zimejengwa huku vyumba vya madarasa zaidi ya 15,000 vipya vya msingi na Sekondari vimejengwa, lakini kama haitoshi kumejengwa shule za awali 1,600 ambazo hazikuwepo hapo awali.

Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amehakikisha amejenga mabweni mapya 1600 ili kuwapunguzia umbali wanafunzi wanaoitafuta elimu ambapo zaidi ya shilingi Trilioni 3.98 zimewekwa kwenye ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ili tu kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Rais Samia ametekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM Ibara ya 80 (i)(a) inayoelekeza Kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu pamoja na kuhifadhi na kuendeleza mazingira ya shule hizo.

 
Halafu cha kushangaza Mishahara ya Walimu imepaa kama kishada, unaambiwa Ualimu unagombewa ni noma!
 
Eilimu
Elimu
Elimu
Na zaidi kaanza kubadili mfumo wa Elimu kuanzia mwaka 2023, kuondoa ule mtaala wa kukaririshana. Mfano elimu ya msingi Sasa kwenda Hadi form 4 kwa maana ya baada ya std 6 watoto wataingia Moja kwa Moja form 1 kwa masomo ya michepuo na stadi za kazi.

Mama anafanya mengi yaliyoshinda wanaume waliomtangulia.

Hongera Dkt Samia.
 
Umezungumzia elimu kwa maana ya majengo tu? Vipi kuhusu walimu, mazingira ya kujifunzia na ubora utokanao na hiyo elimu?
Nitajie watoto wa mawazir watanp wanaosoma kwenye shule zilizo boreshwa na SSH
Nimeshangazwa na mleta mada
 
Eilimu
Elimu
Elimu
Na zaidi kaanza kubadili mfumo wa Elimu kuanzia mwaka 2023, kuondoa ule mtaala wa kukaririshana. Mfano elimu ya msingi Sasa kwenda Hadi form 4 kwa maana ya baada ya std 6 watoto wataingia Moja kwa Moja form 1 kwa masomo ya michepuo na stadi za kazi.

Mama anafanya mengi yaliyoshinda wanaume waliomtangulia.

Hongera Dkt Samia.
Vitabu vipo vya huo mchepuo mpya!? Walimu wamepata mafunzo ya mchepuo mpya?
Nakumbuka tukiwa A LEVEL iliongezwa topic ya Research katika syllabus. Ilikuwa kasheshe kupata mwalimu wa kutufundisa mana waliokuwepo hawakuwa wameisoma hiyo topic. Sasa itakuwaje kwenye mabadiliko ya mtaala TZ?
TUNASHANGILIA KWAKUWA TUNAISHI KWENYE PEPO YA MABWEGE???
 
Back
Top Bottom