Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameizawadia timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Girls’ kiasi cha Sh30 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Unaf huko Tunisia wiki iliyopita.
Fedha hizo zimekabidhiwa Septemba 11, 2024 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro muda mfupi baada ya msafara wa timu hiyo kurejea Tanzania.
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amemshukuru Rais Samia kwa zawadi hiyo kwenda kwa Serengeti Girls huku akiamini zitakuwa chachu katika juhudi za kuhakikisha timu hiyo inatinga fainali za Kombe la Dunia mwaka 2025.
“Hili ni jambo jema lakini nia yetu ni kurudi tena kwenda Kombe la Dunia chini ya miaka 17. Kwa matayarisho haya na jitihada zenu pamoja na walimu tuna uhakika kabisa tutafanikiwa.
“Sisi kama shirikisho bado tunaendelea kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira mazuri ili tuweze kujitayarisha na nia yetu kubwa na adhima yetu ni kwamba mashindano yoyote ambayo yatapatikana na fursa itapatikana tutaenda kushiriki ili kuweza kupata uzoefu.
Tutakapofika kwenye mashindano ya kufuzu ili tuweze kuwa mahiri zaidi kwa sababu unapocheza michezo mingi na unapocheza mashindano ndio unapokuwa imara zaidi,” amesema na kuongeza Karia.
Soma pia:
=> Timu ya Serengeti Girls yaweka rekodi Bungeni leo Juni 07, 2022
=> Bunge latengua kanuni kuruhusu Serengeti Girls kutinga mbele ya Bunge