Rais Samia amemteua Mussa Makame, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri na Uwekezaji wa Mfuko wa Mafuta na Gesi

Yaani honestly speaking 57 trilion cubic feet of Tz Natural gas ni mali ya Western powers it has little impact on our economy ....hii inatokana na mikataba mibovu ambayo tumeingia nao hao western powers ....TPDC wana 14% Only , kwanini Botswana waliweza 50%50% kwenye dimond kwanini sisi tumeshindwa ???????
 
TOKA MAKTABA:

26 September 2019

Rais John Magufuli ameteua mwenyekiti na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board)

Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Dk Leonard Chamriho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Uwekezaji wa Mapato ya Mafuta na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board).

Dk Chamriho ni Katibu Mkuu wa Uchukuzi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Pamoja na uteuzi wa Mwenyekiti, Rais Magufuli amewateua wajumbe wanne wa bodi hiyo ambao ni;
  • Casmir Sumba Kyuki (Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria).
  • Dk Suleiman Magesa Missango (Mkurugenzi wa Utafiti wa Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania – BOT).
  • Safiel Fahamuel Msomvu (Kaimu Meneja Uwekezaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania – TPDC).
  • Dk Mussa Daniel Budeba (Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM).
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Septemba 26, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania imemnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akisema uteuzi wa Dk Chamriho na wajumbe hao ulianza Septemba 25, 2019.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
26 Septemba, 2019
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…