Rais Samia ameongeza Bilioni 654 bajeti Mikopo Elimu ya Juu

Rais Samia ameongeza Bilioni 654 bajeti Mikopo Elimu ya Juu

"Mikopo ni fedha. Tangu shughuli ya kukopesha fedha imeanza miaka 19-20 takriban Tril.7. 3 zimewekezwa. Huu unaitwa ni uwekezaji wa Serikali katika rasilimali watu. Na wanufaika Laki Saba wamepata mikopo.

"Katika miaka Mitano au Sita kuanzia 2020-21 kiasi cha bajeti kilichopitishwa ni Bil. 464 na wanufaika walikuwa Laki na Nusu. Mwaka uliofuata ni Bil. 570

"Wakati Mama, Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia mwaka 2021-22 ameongeza kwa kiasi kikubwa sana kutoka Bil. 464 hadi 570 ni ongezeko kubwa sana na halijafanyika kwa miaka mingi wakanufaika wanafunzi Laki moja na sabini na saba.

"Na mwaka Jana ilikuwa Bil. 654 wanufaika Laki moja na tisini na huu mwaka wanufaika watakuwa Laki mbili na ishirini na bajeti ni Bil.786." Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru

#PBCloudsFM

Acheni propaganda, ada laki mbili ndio mkopo gani?. Shughulikeni na mikopo acheni kujisafisha.
 
Hiki wanachofanya ni siasa zisizo na uhalisia, kuna wanafunzi kibao hawajapewa hiyo mikopo na wengine wana mwezi tangu wamefungua vyuo hakuna pesa waliyoingiziwa, hivi mnaposema uongo ni kwa manufaa ya nani hasa!!??
Kuna mwanafunzi ametokea Kigoma alikuwa anahaha auze simu apate nauli arudi kwao, hizi ni siasa za maji taka
 
Yaani kila mtu alitakiwa kupata sio hini ya milioni tatu. Lakini sasa
 
Back
Top Bottom