Rais Samia amepiga 'hat trick' kwenye Korosho

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Na Emmanuel J. Shilatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepiga 'hat trick' kwenye zao la Korosho katika mambo yaliyokuwa kero na vilio vya siku nyingi vya Wakulima.

I: PEMBEJEO
Rais Samia ametatua kilio cha Wakulima cha pembejeo ambapo Safari hii pembejeo zimeanza kufika kwa wakati.

Sio tu pembejeo kufika kwa wakati bali pia amefuta makato ya Tsh. 110 kwa kila kilogram moja ya Korosho na badala yake mkulima atalipa marejesho kwa idadi ya mifuko aliyochukua. Jambo hili limempunguzia mzigo mkubwa wa malipo Mkulima.

Hajaishia hapo, Rais Samia ameagiza taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo kwa Wakulima na mikopo hiyo ianze kutolewa kwa wakati.

II: USAFIRISHAJI
Rais Samia ameagiza Korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Kitendo hicho kitapunguza gharama na mzunguko mkubwa wa usafirishaji wa Korosho ambapo awali ilibidi wazisafirishe kwa malori mpaka bandari ya Dar es Salaam. Hapa kicheko na furaha kwa Wafanyabiashara na Wakulima, kila pande itaongeza faida ya zao hilo kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji.

III: MKAKATI KUFUTA TOZO
Dhamira nyingine njema ya Rais Samia kwenye zao la Korosho ambapo ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa bandari kupitia na kufuta tozo zote zinazowakwaza Wasafirishaji ili kuwavutia kutumia bandari ya Mtwara. Mwanzo mzuri kuondoa vikwazo vyote vitokanavyo na tozo kwenye zao la Korosho.

Mambo haya mazuri ya kuimarisha sekta ya kilimo yanayoanzwa kufanywa na Rais Samia, yamulike pia kwenye mazao yote mengineyo ili Watanzania waone umuhimu na kuongeza juhudi kwenye kilimo cha biashara ambacho kitasaidia kuongeza pato binafsi la Mkulima na pato la Taifa.

Shilatu, E.J
 
Dhamira njema ya Mama italikomboa taifa, tofauti na mwendazake alitanguliza mitazamo yake sahihi ama vinginevyo hivyo wataalamu na watendaji kupata wakati mgumu kutekeleza inline na mitazamo ya mtawala.
 
SSH mikumi tena ,mama ubarikiwe umeme 27000/= Tanzania nzima Single Phase....Kuna watu walikuwa wana mindset kwamba sisi ni watu wa kupinga ,ukifanya jambo zuri lazima upongezwe ,sasa mtu unapiga risasi raia ,unaua watu unataka tukusifie kwakuwa unajenga flyover na sgr?
 
Hingera sana mama ,Mh Raisi mama samia jimbo letu la same lina shida kumbwa yakuunganishishiwa umeme mfano kata nzima ya lugulu haina umeme tukuombd mh Samia utukumbuke katika hili.
Kero ya pili ni miundombinu ya barabara haipitiki mfano barabara za milimani nishida tupu hazipitiki tunaomba utuangalia mama
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepiga 'hat trick' kwenye zao la Korosho katika mambo yaliyokuwa kero na vilio vya siku nyingi vya Wakulima.

I: PEMBEJEO
Rais Samia ametatua kilio cha Wakulima cha pembejeo ambapo Safari hii pembejeo zimeanza kufika kwa wakati.

Sio tu pembejeo kufika kwa wakati bali pia amefuta makato ya Tsh. 110 kwa kila kilogram moja ya Korosho na badala yake mkulima atalipa marejesho kwa idadi ya mifuko aliyochukua. Jambo hili limempunguzia mzigo mkubwa wa malipo Mkulima.

Hajaishia hapo, Rais Samia ameagiza taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo kwa Wakulima na mikopo hiyo ianze kutolewa kwa wakati.

II: USAFIRISHAJI
Rais Samia ameagiza Korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Kitendo hicho kitapunguza gharama na mzunguko mkubwa wa usafirishaji wa Korosho ambapo awali ilibidi wazisafirishe kwa malori mpaka bandari ya Dar es Salaam. Hapa kicheko na furaha kwa Wafanyabiashara na Wakulima, kila pande itaongeza faida ya zao hilo kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji.

III: MKAKATI KUFUTA TOZO
Dhamira nyingine njema ya Rais Samia kwenye zao la Korosho ambapo ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa bandari kupitia na kufuta tozo zote zinazowakwaza Wasafirishaji ili kuwavutia kutumia bandari ya Mtwara. Mwanzo mzuri kuondoa vikwazo vyote vitokanavyo na tozo kwenye zao la Korosho.

Mambo haya mazuri ya kuimarisha sekta ya kilimo yanayoanzwa kufanywa na Rais Samia, yamulike pia kwenye mazao yote mengineyo ili Watanzania waone umuhimu na kuongeza juhudi kwenye kilimo cha biashara ambacho kitasaidia kuongeza pato binafsi la Mkulima na pato la Taifa.

Shilatu, E.J
Nilitegemea kwenye hizo hut-trick kuna bei ya korosho ambayo inategemewa.....swala la kutumia bandari ya mtwara sio geni na sio mara ya kwanza na wasafirishaji ndio huamua pakupitishia bidhaa yao.
Mara ya mwisho kabisa korosho iliuzwa kwa zaidi ya 3500 kwa kilo ..sasa tuna tarajia zaidi ya hapo sio wanakuja na bei ya 1200 kwa wakulima lazima tutawauliza mnashangilia nini?
 
ikifika mwezi wa Tisa naenda zangu Masasi mapema Kwenye msimu wa korosho.... asante Sana mama Kwa kutukumbuka Sisi wakulima
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepiga 'hat trick' kwenye zao la Korosho katika mambo yaliyokuwa kero na vilio vya siku nyingi vya Wakulima.

I: PEMBEJEO
Rais Samia ametatua kilio cha Wakulima cha pembejeo ambapo Safari hii pembejeo zimeanza kufika kwa wakati.

Sio tu pembejeo kufika kwa wakati bali pia amefuta makato ya Tsh. 110 kwa kila kilogram moja ya Korosho na badala yake mkulima atalipa marejesho kwa idadi ya mifuko aliyochukua. Jambo hili limempunguzia mzigo mkubwa wa malipo Mkulima.

Hajaishia hapo, Rais Samia ameagiza taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo kwa Wakulima na mikopo hiyo ianze kutolewa kwa wakati.

II: USAFIRISHAJI
Rais Samia ameagiza Korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Kitendo hicho kitapunguza gharama na mzunguko mkubwa wa usafirishaji wa Korosho ambapo awali ilibidi wazisafirishe kwa malori mpaka bandari ya Dar es Salaam. Hapa kicheko na furaha kwa Wafanyabiashara na Wakulima, kila pande itaongeza faida ya zao hilo kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji.

III: MKAKATI KUFUTA TOZO
Dhamira nyingine njema ya Rais Samia kwenye zao la Korosho ambapo ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa bandari kupitia na kufuta tozo zote zinazowakwaza Wasafirishaji ili kuwavutia kutumia bandari ya Mtwara. Mwanzo mzuri kuondoa vikwazo vyote vitokanavyo na tozo kwenye zao la Korosho.

Mambo haya mazuri ya kuimarisha sekta ya kilimo yanayoanzwa kufanywa na Rais Samia, yamulike pia kwenye mazao yote mengineyo ili Watanzania waone umuhimu na kuongeza juhudi kwenye kilimo cha biashara ambacho kitasaidia kuongeza pato binafsi la Mkulima na pato la Taifa.

Shilatu, E.J
Nikajua Mama kawalipa wale wote waliodhurumiwa pesa zao za korosho na Mwendawazimu .
Kumbe kelele tu zakutaka teuzi, hovyooo..!
 
Back
Top Bottom