Rais Samia amepiga 'hat trick' kwenye Korosho

Rais Samia amepiga 'hat trick' kwenye Korosho

Mwendazake kwa umbumbumbu wake aliharibu mifumo ya biashara ya korosho huko kusini.
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepiga 'hat trick' kwenye zao la Korosho katika mambo yaliyokuwa kero na vilio vya siku nyingi vya Wakulima.

I: PEMBEJEO
Rais Samia ametatua kilio cha Wakulima cha pembejeo ambapo Safari hii pembejeo zimeanza kufika kwa wakati.

Sio tu pembejeo kufika kwa wakati bali pia amefuta makato ya Tsh. 110 kwa kila kilogram moja ya Korosho na badala yake mkulima atalipa marejesho kwa idadi ya mifuko aliyochukua. Jambo hili limempunguzia mzigo mkubwa wa malipo Mkulima.

Hajaishia hapo, Rais Samia ameagiza taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo kwa Wakulima na mikopo hiyo ianze kutolewa kwa wakati.

II: USAFIRISHAJI
Rais Samia ameagiza Korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Kitendo hicho kitapunguza gharama na mzunguko mkubwa wa usafirishaji wa Korosho ambapo awali ilibidi wazisafirishe kwa malori mpaka bandari ya Dar es Salaam. Hapa kicheko na furaha kwa Wafanyabiashara na Wakulima, kila pande itaongeza faida ya zao hilo kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji.

III: MKAKATI KUFUTA TOZO
Dhamira nyingine njema ya Rais Samia kwenye zao la Korosho ambapo ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa bandari kupitia na kufuta tozo zote zinazowakwaza Wasafirishaji ili kuwavutia kutumia bandari ya Mtwara. Mwanzo mzuri kuondoa vikwazo vyote vitokanavyo na tozo kwenye zao la Korosho.

Mambo haya mazuri ya kuimarisha sekta ya kilimo yanayoanzwa kufanywa na Rais Samia, yamulike pia kwenye mazao yote mengineyo ili Watanzania waone umuhimu na kuongeza juhudi kwenye kilimo cha biashara ambacho kitasaidia kuongeza pato binafsi la Mkulima na pato la Taifa.

Shilatu, E.J
Kwa hiyo rais mwanamke kamshinda rais wakiume! Hopeless kabisa nyie wafuasi wa dikteta marehemu
 
na kwa haraka tu barabara ya mzunguko imekufa iliyokuwa ibadili sura ya Dodoma
nani amekwambia imekufa wakati mwezi jana watu wamelipwa pesa ili wapishe huo ujenzi ambao tayari umeshaanza. Acha kuongea vitu usivyovijua
 
Kwani bado kulipwa ? Mabomu yako wapi walipue korosho zibanguliwe bei ya serikali ??
 
Suala la korosho lilikuwa linahitaji akili sana kuliko maguvu

Mama anaendelea kuchukua point 3 ukilinganisha na mtangulizi wake.
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepiga 'hat trick' kwenye zao la Korosho katika mambo yaliyokuwa kero na vilio vya siku nyingi vya Wakulima.

I: PEMBEJEO
Rais Samia ametatua kilio cha Wakulima cha pembejeo ambapo Safari hii pembejeo zimeanza kufika kwa wakati.

Sio tu pembejeo kufika kwa wakati bali pia amefuta makato ya Tsh. 110 kwa kila kilogram moja ya Korosho na badala yake mkulima atalipa marejesho kwa idadi ya mifuko aliyochukua. Jambo hili limempunguzia mzigo mkubwa wa malipo Mkulima.

Hajaishia hapo, Rais Samia ameagiza taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo kwa Wakulima na mikopo hiyo ianze kutolewa kwa wakati.

II: USAFIRISHAJI
Rais Samia ameagiza Korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Kitendo hicho kitapunguza gharama na mzunguko mkubwa wa usafirishaji wa Korosho ambapo awali ilibidi wazisafirishe kwa malori mpaka bandari ya Dar es Salaam. Hapa kicheko na furaha kwa Wafanyabiashara na Wakulima, kila pande itaongeza faida ya zao hilo kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji.

III: MKAKATI KUFUTA TOZO
Dhamira nyingine njema ya Rais Samia kwenye zao la Korosho ambapo ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa bandari kupitia na kufuta tozo zote zinazowakwaza Wasafirishaji ili kuwavutia kutumia bandari ya Mtwara. Mwanzo mzuri kuondoa vikwazo vyote vitokanavyo na tozo kwenye zao la Korosho.

Mambo haya mazuri ya kuimarisha sekta ya kilimo yanayoanzwa kufanywa na Rais Samia, yamulike pia kwenye mazao yote mengineyo ili Watanzania waone umuhimu na kuongeza juhudi kwenye kilimo cha biashara ambacho kitasaidia kuongeza pato binafsi la Mkulima na pato la Taifa.

Shilatu, E.J
Lipi jipya Hapo?
Je korosho ikisafirishwa kupitia mtwara ndio mkulima hatalipa gharama za usafirishaji?

Je ni wapi umeongelea Rais kupata Soko la uhakika la korosho ambayo ndio kero kubwa ya wakulima.
Hayo makato yote aliyoondoa ndio hayo aliyokuwa akiyakataa #JPM.
Ni makato yanayowanufaisha zaidi wabunge kina Nape kukopeshana fwedha za Bodi za mazao ya wakulima
 
Sio kwa style ya mtwara lakini
Wenye kangomba hawapori korosho, wala hawaibi korosho toka kwa wananchi. Wananchi huuza korosho kwa hiari yao kwa wenye kangomba ili wapate mahitaji yao ikiwamo fedha za pembejeo za korosho.

Kumbuka wananchi hawa hawana mjomba wa kuwapatia fedha za mahitaji hayo, maana ni dunia ya kibebari.
 
Mwaka huu bei ya korosho itakuwa nzuri,kumi tena kwa mama,nasema uongo ndugu zangu
 
𝙽𝚊𝚘𝚖𝚋𝚊 𝚞𝚒𝚠𝚎𝚔𝚎 𝚜𝚊𝚠𝚊 𝚝𝚊𝚊𝚛𝚒𝚏𝚊 𝚢𝚊𝚔𝚘 𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚑𝚊𝚙𝚘 𝚊𝚠𝚊𝚕𝚒 𝚑𝚊𝚒𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚕𝚊𝚣𝚒𝚖𝚊 𝚔𝚞𝚜𝚊𝚏𝚒𝚛𝚒𝚜𝚑𝚒𝚊 𝚋𝚊𝚗𝚍𝚊𝚛𝚒 𝚢𝚊 𝙳𝙰𝚁 𝚒𝚕𝚊 𝚠𝚊𝚗𝚞𝚗𝚞𝚣𝚒 𝚠𝚎𝚗𝚢𝚎𝚠𝚎 𝚠𝚊𝚕𝚒𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚠𝚊𝚗𝚊𝚠𝚎𝚣𝚊 𝚔𝚞𝚌𝚑𝚊𝚐𝚞𝚊 𝚠𝚊𝚙𝚒 𝚠𝚊𝚜𝚊𝚏𝚒𝚛𝚒𝚜𝚑𝚒𝚎 𝚖𝚒𝚣𝚒𝚐𝚘 𝚢𝚊𝚘 𝚒𝚕𝚊 𝚢𝚎𝚢𝚎 𝚂𝙰𝙼𝙸𝙰 𝚔𝚊𝚠𝚎𝚔𝚊 𝚜𝚑𝚊𝚛𝚝𝚒 𝚔𝚞𝚠𝚊 𝚕𝚊𝚣𝚒𝚖𝚊 𝚣𝚒𝚜𝚊𝚏𝚒𝚛𝚒𝚜𝚑𝚒𝚎 𝙼𝚃𝚆𝙰𝚁𝙰 𝙿𝙾𝚁𝚃 𝚗𝚊 𝚜𝚒 𝚔𝚠𝚒𝚗𝚐𝚒𝚗𝚎 𝚔𝚘𝚔𝚘𝚝𝚎 𝚒𝚕𝚊 𝚋𝚊𝚗𝚍𝚊𝚛𝚒 𝚣𝚘𝚝𝚎 2 𝚣𝚒𝚔𝚒𝚝𝚞𝚖𝚒𝚔𝚊 𝚔𝚊𝚋𝚕𝚊 𝚔𝚞𝚜𝚊𝚏𝚒𝚛𝚒𝚜𝚑𝚒𝚊 𝚔𝚘𝚛𝚘𝚜𝚑𝚘 𝚢𝚊𝚊𝚗𝚒 𝚢𝚊 𝙼𝚝𝚠𝚊𝚛𝚊 𝚗𝚊 𝚢𝚊 𝙳𝙰𝚁.
 
Ndiyo. Ushirika wa nn ktk zama hizi za biashara mtandao (e-commerce)??
Mambo ya ushirika yamepitwa na wakati...PM anakazania SANA kukamilisha ilani, kwa kuhakikisha mazao analyzes kwenye ushirika kwa sababu eti kumlinda mkulima, ila ukija kuchunguza ni kuikusanyia serikali mapato, TRA, TARURA, VIPIMO, sijui mazingira e.t.c

Hatukatai tozo ila ka hakuna huduma zinaudhi.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Kura za Lindi na Mtwara hazina madhara, ukitaka ushindi wowote lazima upate kanda ya Ziwa, Dsm, nyanda za juu na kanda ya Kati.
Wewe muongo,hata ukose kura Dar kanda ya ziwa na kanda ya kati ushindi utakuwa wako tu muhimu uwe na polisi na tume inayoongozwa na wachumia tumbo dizain ya kicheere!!!

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Angekuwa. Mwendazake angepiga pambio nchi nzima huku vibwengo wake wakichagiza.

Mama anakimbiza mwizi kimya kimya katoa mil.500 za ujenzi wa barabara kwa kila jimbo via Tarura juu ya bajeti ya kawaida
 
Wenye kangomba hawapori korosho, wala hawaibi korosho toka kwa wananchi. Wananchi huuza korosho kwa hiari yao kwa wenye kangomba ili wapate mahitaji yao ikiwamo fedha za pembejeo za korosho.

Kumbuka wananchi hawa hawana mjomba wa kuwapatia fedha za mahitaji hayo, maana ni dunia ya kibebari.
Mnachekesha sana watu mnaosapoti ushirika kufutwa! Mnatumia shida za watu kuwakandamiza.
 
Back
Top Bottom