Rais Samia amepiga 'hat trick' kwenye Korosho

Rais Samia amepiga 'hat trick' kwenye Korosho

nani amekwambia imekufa wakati mwezi jana watu wamelipwa pesa ili wapishe huo ujenzi ambao tayari umeshaanza. Acha kuongea vitu usivyovijua
saamahani boss wangu nimekoma mimi!
1623141615576.png
 
Enzi hizo alipokuwa anaupiga mwingi, sasa hivi anabutuabutua tu.

serikali yake imejaa uonevu mkubwa dhidi ya upinzani na wapinzani nchini.
Haheshimu katibu na kiaoo chake kwenye suala la haki za kisiasa nchini
 
"Problems cannot be solved by the same level of thinking that created them in the first place".
 
Dhamira njema ya Mama italikomboa taifa, tofauti na mwendazake alitanguliza mitazamo yake sahihi ama vinginevyo hivyo wataalamu na watendaji kupata wakati mgumu kutekeleza inline na mitazamo ya mtawala.
Bro, ukimsifu mama si lazima ufananishe na utawala wa jiwe, hio itatuaminisha kuwa jiwe ameweka viwango vya kutumika Kama reference ktk utawala
Naomba nikukumbushe kuwa jiwe ndiye aliyekomboa korosho. Enzi hizo tulikuwa tunauziana bukubuku, na Mara alipoingia jiwe Bei ikapaa Hadi 4000, wanakusini tunakumbuka Hilo.
Malalamiko makubwa yakaibuka kutoka kwa wafanya biashara ambao walikuwa wananufaika hapo awali
Mama anaendeleza kuboresha tu kwa kutatua kero ndogondogo zilizopo, na hatazimaliza, na hata utawala ujao wataendeleza
Basi sema yeye ni Bora kuliko Marais wote maana anachofanya hawakufanya
 
Na Emmanuel J. Shilatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepiga 'hat trick' kwenye zao la Korosho katika mambo yaliyokuwa kero na vilio vya siku nyingi vya Wakulima.

I: PEMBEJEO
Rais Samia ametatua kilio cha Wakulima cha pembejeo ambapo Safari hii pembejeo zimeanza kufika kwa wakati.

Sio tu pembejeo kufika kwa wakati bali pia amefuta makato ya Tsh. 110 kwa kila kilogram moja ya Korosho na badala yake mkulima atalipa marejesho kwa idadi ya mifuko aliyochukua. Jambo hili limempunguzia mzigo mkubwa wa malipo Mkulima.

Hajaishia hapo, Rais Samia ameagiza taasisi za kifedha kutoa mikopo ya pembejeo kwa Wakulima na mikopo hiyo ianze kutolewa kwa wakati.

II: USAFIRISHAJI
Rais Samia ameagiza Korosho zote zinazozalishwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara kwani Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika bandari hiyo kwa kuikarabati na kuipanua.

Kitendo hicho kitapunguza gharama na mzunguko mkubwa wa usafirishaji wa Korosho ambapo awali ilibidi wazisafirishe kwa malori mpaka bandari ya Dar es Salaam. Hapa kicheko na furaha kwa Wafanyabiashara na Wakulima, kila pande itaongeza faida ya zao hilo kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji.

III: MKAKATI KUFUTA TOZO
Dhamira nyingine njema ya Rais Samia kwenye zao la Korosho ambapo ametoa maelekezo kwa viongozi wote wa bandari kupitia na kufuta tozo zote zinazowakwaza Wasafirishaji ili kuwavutia kutumia bandari ya Mtwara. Mwanzo mzuri kuondoa vikwazo vyote vitokanavyo na tozo kwenye zao la Korosho.

Mambo haya mazuri ya kuimarisha sekta ya kilimo yanayoanzwa kufanywa na Rais Samia, yamulike pia kwenye mazao yote mengineyo ili Watanzania waone umuhimu na kuongeza juhudi kwenye kilimo cha biashara ambacho kitasaidia kuongeza pato binafsi la Mkulima na pato la Taifa.

Shilatu, E.J
1. Pembejeo-amekuta mipango hiyo tayari ilikuwa iko kwenye utekelezaji hivyo ni uongo kudai kafanikisha yeye wakati katekeleza mpango uliokuwepo. Makampuni kadhaa ya uzalishaji na usambazaji mbolea na dawa tayari zilikuwa zimeshaanza kuandaa maghala Mtwara mjini, Tunduru na Nachingwea kwa hiyo madai yako sio sahihi
2.Usafirishaji-uwekezaji wa bandari ulishakamilishwa na mtangilizi wake sio yeye kuhusu usafirishaji wa maji na barabara hizo zote zilikuwa tayari zimeshakamilika yeye anatekelezaji kilichokuwemo kwenye mipango hakuna jipya
3.TOZO miamala-hakuna cha maana kilichofanyika kupunguza au kuondosha kabisa na kuhamishia kwingine upatikanaji wa mapato pasipo kuumiza wananchi. Kutuma laki moja makato ni karibu gharama ya shili elfu tatu; wakati mpokeaji anakatwa shilingi 5,500-6,000/- hapo nafuu iko wapi?
3.
 
Mama yuko vizuri, anafanya kazi nzuri sana!
Report ya BOT, mauzo ya korosho yameshuka kuliko kawaida, USD mil 159
Sasa nikisoma hii post na hizi replies noana shida kwa hawa chawa wa CCM.
Kuna kipindi wakasema kampuni ya marekani itanunua korosho zote. Sijui nn kimetokea
Ila wakulima bongo watakuwa wanachezeshwa kila ngoma na wanasiasa,
 
Back
Top Bottom