Beberu
JF-Expert Member
- Jan 26, 2017
- 4,548
- 9,740
Kwa hio hao masikin watibiwe bure ? Wasitoe chochote? Wao kazi yao kwenye hili taifa ni ipi? Hao wenye pesa walipewa bure? Watu wafanya biashara wataokatwa pesa za electronic transfer wao walipewa bure?Mkuu ukichukua 2,000 ya masikini inauma zaidi kuliko kuchukua 2,000,000 ya tajiri. Ukirudia kusoma uzi kwa makini utaelwa hoja yangu.
Acheni ku glorify umaskini, mtu upo kwenye taifa unataka upewe kila kitu bure, wew mchango wako ni upi kama hata kukatwa 2000/- kwa mwezi kwenye electronic money transfer ili ugharamie matibabu yako huwezi?
Watu kama hao bora wahamie Burundi, ila ukweli kila mtu abebe mzigo wake, Binafs naona serikali kuhusu bima kwa wote inazingua, inachotakiwa kufanya ni kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kwa kila mtu na bei ambayo ni rafiki kwa watanzania wengi,
Hivyo napendekeza
#1. Malipo yawe kwa mwezi, isiwe lazima mtu kulipa hela yote kwa mkupuo
#2. Watu wakijiunga kupitia vikundi wapunguziwe kadri kundi linavyozidi kuwa kubwa
Kulipiana bima ni kuzalisha kizazi cha wavivu wanaopenda kifanyiwa kila kitu