Rais Samia amerejea kuomboleza msiba wa Hanang au amekuja kutuhamishia Burundi?

Mkuu ukichukua 2,000 ya masikini inauma zaidi kuliko kuchukua 2,000,000 ya tajiri. Ukirudia kusoma uzi kwa makini utaelwa hoja yangu.
Kwa hio hao masikin watibiwe bure ? Wasitoe chochote? Wao kazi yao kwenye hili taifa ni ipi? Hao wenye pesa walipewa bure? Watu wafanya biashara wataokatwa pesa za electronic transfer wao walipewa bure?

Acheni ku glorify umaskini, mtu upo kwenye taifa unataka upewe kila kitu bure, wew mchango wako ni upi kama hata kukatwa 2000/- kwa mwezi kwenye electronic money transfer ili ugharamie matibabu yako huwezi?

Watu kama hao bora wahamie Burundi, ila ukweli kila mtu abebe mzigo wake, Binafs naona serikali kuhusu bima kwa wote inazingua, inachotakiwa kufanya ni kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kwa kila mtu na bei ambayo ni rafiki kwa watanzania wengi,
Hivyo napendekeza

#1. Malipo yawe kwa mwezi, isiwe lazima mtu kulipa hela yote kwa mkupuo

#2. Watu wakijiunga kupitia vikundi wapunguziwe kadri kundi linavyozidi kuwa kubwa


Kulipiana bima ni kuzalisha kizazi cha wavivu wanaopenda kifanyiwa kila kitu
 
Mkuu umeongea vema. Serikali imekosea big time. Nchi inapuyanga tu kama kipepeo. Hii ndio hasara ya kuongozwa na mijitu isiyokwenda shule.
 
Njia mbdala?
 
Mkuu umeongea vema. Serikali imekosea big time. Nchi inapuyanga tu kama kipepeo. Hii ndio hasara ya kuongozwa na mijitu isiyokwenda shule.
Kwa kiasi imekosea, sema tusimalize maneno, tusubiri sheria na sera zinazokuja sasa,
Ila am sure hao wataopewa bima za bure zitakuwa ni za ovyo, zitakuwa za kumuona Dr. Na hazina vipimo vingi na dawa nyingi, ukitaka ya uhakika ni kulipia
 
Iv kwa mfano ww ni mkuu wa kaya wanakutegemea kwa kila kitu lakini haufanyi kazi, kazi yako kuzurura na kuuza kilichopo home kisha kukitokea mmoja wa wanafamilia kupata shida au kufariki,ndo unarudi home na unajifanya umesktishwa na kifo na kutoa msaada,na wanafamilia wakakushangilia kuwa ndo mkuu wa kaya mwema. hii imekaaje, ngoja tu niixhie apa
 
Umeona eeh? Hii ni shida sana mkuu. Nashangaa muathirika mmoja wa mafuriko amepewa msaada kule Hanang amemshukuru Rais kuleta tope limesababisha amepata msaada. Nchi hii ina watu wa ajabu sana aisee!
 
Umeona eeh? Hii ni shida sana mkuu. Nashangaa muathirika mmoja wa mafuriko amepewa msaada kule Hanang amemshukuru Rais kuleta tope limesababisha amepata msaada. Nchi hii ina watu wa ajabu sana aisee!
mungu anisaidie nikue nizae niwe mkuu wa kaya mbona mashamba yote alokodisha bibi nawakabidhi wanakaya iwe mali yao kama wataamua kuyalima watalima kama hawalimi yatabak hvo hvo si ni mali yao kwan lazima kukodisha?
 
"" Watanzania tunakamuliwa mno!

Viongozi wa nchi hii wamekosa ubunifu. Wanajiendea tu kama vipepeo wasiokuwa na dira wala muelekeo. Nchi ingekuwa na watu wanaofikiri sawasawa, wasingekuja na hoja ya kutaka kuwakamua wananchi zaidi wakati wananchi hao hao wanaendelea kukamuliwa kodi ya kizalendo isiyokuwa na kichwa wala miguu. Haya ndiyo matokeo ya kutawaliwa na watu wasiokuwa na dira wala muelekeo. Wanapuyanga tu bora liende.

Nawasilisha."" [emoji3596]
NMEKUELEWA VYEMA
 
Wapunguze seminar na washa zimezidi.Viongozi wapunguze safari na misururu ya watu wanaoambatana nao nchiza nje. mabalozi watumike.Mashangingi yasitumike
 
Kama nani? Pendekeza nitawaomba wasi mkolimbe.
Acha utani. Nchi hii inahitaji uongozi thabiti siyo maigizo. Nitakupa majina tutakapoambiwa Watanzania wenye nia wajitokeze. Kumbuka wale wenye IQ na uwezo wa kuongoza huwa hawataki kupewa madaraka. Hao ndiyo itabidi tuwaombe wajitolee ingawa wao hawapendi kuingia kwenye usanii (siasa)!
 
Mkuu
Mkuu, labda tuelezane kidogo;
1. Ulitaka wapewe unafuu gani kwa mfano? Wa kutibiwa bure kabisa sio? Na kama jibu lako ni ndio je hizo dawa zitanunuliwa kwa pesa ya kina nani?
Kwa maoni yangu bure inayoongelewa hapa ni bure ya insurance baada ya mimi, wewe na Yule kukatwa kodi na may be hata mwaka mzima ukaisha na hatujafika hospital.
Pia kuna wale watakaohitaji matibabu say ya million 20 wakat yeye kwenye tozo zake za simu labda amechangia 1,500 tu. Huoni hapo huyo ametibiwa bure?

2. Nafasi za ajira hazitengenezwi bila kuwa na uchumi imara ambao hutengenezwa na mambo mengi kama vile sera bora za uwekezaji, workforce (ambayo Tunayo) pia mazingira safi ya kiuchumi yatakayovutia wawekezaji. Tunatakiwa sisi tudai mazingira bora yatakayofungua fursa na sio kudai serikali iajiri….hebu jiulize iajiri ili kuzalisha nini? Kumbuka ajira ni fixed cost kwenye mambo ya uchumi.

3. Mwigulu anaangukia katika hoja yangu ile ya mafisadi wote wakamatwe, mali zao zitaifishwe na jela iwahusu.

Bottom line, watanzania tuache kulia lia, serikali sio mama yako au baba yako ikupatie vya bure tuuu! Sera nyingi kama siasa ni kilimo, kazi ni kipimo cha utu nk nk zilikuwa ni katika lengo la kuwaamsha wananchi wajenge nchi yao but cha ajabu mpaka sasa wapo wanaotaka vya bure a.k.a DEZOOOO
 
Mkuu ukichukua 2,000 ya masikini inauma zaidi kuliko kuchukua 2,000,000 ya tajiri. Ukirudia kusoma uzi kwa makini utaelwa hoja yangu.
Nani alikuambia hivo mkuu? Kwani yeye huyo tajiri ameokota hiyo pesa?
 
Kwani Kasharudi, lini.
 
Nani alikuambia hivo mkuu? Kwani yeye huyo tajiri ameokota hiyo pesa?
Matajiri wanapata pesa kwa masikini kwa kuwafanyisha kazi za cheap labour na kuwapandishia bei ya bidhaa kiholela. Kwa mfano unakuta serikali inaongeza kodi ya Tsh 100 kwa lita lakini tajiri anatumia kigezo hicho kupandisha nauli kwa Tsh 500 kwa kichwa. Wee huoni kuwa hapo masikini amekamuliwa mno?
 
Tatizo mkuu cjui watz tulilishwa Nini eti!.
Kuna wanavijiji wanatia kichefuchefu Haki ya nani.
Mfano,matatizo yaliyopo ya kimkakati bado wanapiga magoti kwa viongozi WA CCM eti wawasaidie miaka nenda Rudi.Hata ile kujiuliza Serikali inayoo gozwa na chama tangu uhuru ndo ile ile.
Kujiongeza hakuna,Kama mazumbukuku.Kina Tundu lisu Hadi wanachoka mkuu.
Mijitu inatetewa,lakini yapoe CCM miaka dahari na maisha no change.balabala,maji,hakuna.
Inqfikirisha.
Angalau mjini wanamwamko,ila vijijini ndo watu wengi wako kule.
Mungu alituepushia siasa zile zilizokuwa zinachipua kwa Kasi ya ajabu ya kuzimwa sauti mbadala eti zinakwamisha maendeleo😠😠😠.
Ukijiuliza Toka lini wapinzani walio gozwa Serikali ni lini hupati jibu.
Na bado mijitu inashangilia kwa shwangwe kulekule.Me nimpenzi WA Democrasia,kwa maana huamsha mengi.
 
Hii nchi watu wanadhani wanaidai nchi/serikali vitu vya bure, et mnalalamikia kugharamia bima ya Afya hahah
 
Hii nchi watu wanadhani wanaidai nchi/serikali vitu vya bure, et mnalalamikia kugharamia bima ya Afya hahah
Ni ajabu sana mkuu! Yaan watu wanataka vya bure tu…. Malalamiko yao ni serikali iwasaidie tu bila wao kuchangia maendeleo
 
Ni ajabu sana mkuu! Yaan watu wanataka vya bure tu…. Malalamiko yao ni serikali iwasaidie tu bila wao kuchangia maendeleo
Kwani hizo fedha ambazo wananchi wanaomba serikali "iwasidie" huwa serikali inaziokota wapi wakati hizo ni KODI zao wananchi?

Serikali inakusanya kodi kutoka kwa wananchi, hivyo ni lazima izirejeshe kodi hizo kwa wananchi kwa kuwaboreshea huduma za jamii. Hii sio hisani kwani fedha zote za serikali zinatoka ama kwa wananchi au kwa kuuza rasilimali za watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…