Rais Samia amerejesha uendeshaji shughuli za Serikali kwa uwazi

Rais Samia amerejesha uendeshaji shughuli za Serikali kwa uwazi

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Hii ni habari njema sana kwa Watanzania wote.

Uongozi wa Rais Samia Suluhu ni uongozi ambao Watanzania wengi tulitamani kuwa nao, ni uongozi tuliokuwa tunauota kwa zaidi ya miaka 5. Tulitamani sana kuwa na uongozi unaofanya shughuli zote kwa uwazi lakini haikuwezekana kwa zaidi ya miaka 5, sijui serikali ilikuwa inaficha maovu gani.

Lakini sasa tupo katika uongozii wenye neema, Tanzania inarudi katika Mpango wa Uendeshaji Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership) baada ya kujitoa mwaka 2017.

Rais Samia Suluhu ni mfano mzuri wa kiongozi bora na sasa amefanikiwa kuimarisha Demokrasia, haki za binadamu na utawala bora.

Uwazi bila maamuzi ni upuuzi

USSR
Unaongelea maamuzi gani hii serikali sio ya kukurupuka mzee lazima ifuate sheria na katiba ya nchi inavyosema lakini kila mwenye kosa lazima awajibishwe kulingana na sheria hii serikali haikumbatii uozo
 
Hii ni habari njema sana kwa watanzania wote.

Uongozi wa Rais Samia Suluhu ni uongozi ambao watanzania wengi tulitamani kuwa nao, ni uongozi tuliokua tunauota kwa zaidi ya miaka 5 Tulitamani sana kuwa na uongozi ...
Mbona wezi hawajulikani na wamepiga mabilioni kama kuna uwazi.

Au unaongelea uwazi upi wewe. Kama ni uwazi wa watu kupenya na kuiba hapo sawa
 
Mbona wezi hawajulikani na wamepiga mabilioni kama kuna uwazi.

Au unaongelea uwazi upi wewe. Kama ni uwazi wa watu kupenya na kuiba hapo sawa
Wezi lazima watajulikana na watawajibishwa kwa uwazi kabisa
 
Naona raisi mwenywewe ndo mwizi
Amekuibia nini au unaropoka tuu mzee

Angekua mwizi asingeruhusu uwazi hata katika ripoti ya SAG kuna mengine lazima yangefichwa
yani uongozi huu ni wa neema aisee watanzania tulitamani sana kufikia hii stage
 
Tena upuuzi unakuwa wa kiwango cha phd kabisa. Sasa akiwaita stupid hapo ndio kawajibika tayari 🤣🤣😀😁
Serikali lazima ifuate sheria haiwezi kufanya mambo kama wewe unavyotaka
 
Hii ni habari njema sana kwa Watanzania wote.

Uongozi wa Rais Samia Suluhu ni uongozi ambao Watanzania wengi tulitamani kuwa nao, ni uongozi tuliokuwa tunauota kwa zaidi ya miaka 5. Tulitamani sana kuwa na uongozi unaofanya shughuli zote kwa uwazi lakini haikuwezekana kwa zaidi ya miaka 5, sijui serikali ilikuwa inaficha maovu gani.

Lakini sasa tupo katika uongozii wenye neema, Tanzania inarudi katika Mpango wa Uendeshaji Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership) baada ya kujitoa mwaka 2017.

Rais Samia Suluhu ni mfano mzuri wa kiongozi bora na sasa amefanikiwa kuimarisha Demokrasia, haki za binadamu na utawala bora.

View attachment 2578622
Na majizi ya pesa za umma ndio yametamalaki !! Na ndio yanayomuharibia maana ni sawasawa na kujitahidi kujaza maji ndoo yenye matundu matundu !!
 
Hii nchi ikiwa na wajinga wengi kama huyu mtoa mada kupata maendeleo ni ndoto.
 
Back
Top Bottom