SI KWELI PreGE2025 Rais Samia amesema pesa ilizochangiwa CCM zitatumika bilioni 20 zingine zitatumika kufanya sherehe baada ya kushinda uchaguzi

SI KWELI PreGE2025 Rais Samia amesema pesa ilizochangiwa CCM zitatumika bilioni 20 zingine zitatumika kufanya sherehe baada ya kushinda uchaguzi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
RAISSAMIA15.AG2025.jpg
 
Tunachokijua
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Januari 19, 2025 ulimpitisha kuwa mgombea wa nafasi ya Urais huku Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea Urais wa Zanzibar.

Baadaye mwezi Agosti 9, 2025 Dkt. Samia alichukua fomu ya kugombea Urais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) akiongozana na mgombea mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambao wanajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Aidha Agosti 12, 2025 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilifanya harambee ya kuchangia Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wawakilishi, Wabunge na Urais ambapo ilifanikiwa kuchangisha Fedha zaidi ya Shilingi Billioni 86.

Madai

Ipo picha iliyochapishwa katika kikundi cha mtandao wa Facebook na mtu mwenye anayetumia jina la 'Mchochezi wa haki' ikiwa na ujumbe unaoonekana kuchapishwa na Rais Samia kwenye ukurasa wake wa X ukisema 'pesa ilizochangiwa CCM zitatumika bilioni 20 zingine zitatumika kufanya sherehe baada ya kushinda uchaguzi'

Je, ni upi uhalisia wa ujumbe huo?


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujachapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Rais Samia kupitia mtandao wa X.

Aidha ujumbe huo una mapungufu yanayodhihirisha kuwa ni wa kutengenezwa na wapotoshaji. Picha yenye ujumbe huo haiakisi uhalisia kama ilivyo katika mtandao wa X, mfano kutumika kwa tiki ya bluu (blue checkmark) badala ya tiki yenye rangi ya kijivu (Grey checkmark) ambayo inatumiwa na Rais Samia.

Kukosekana kwa alama ya Grok, nukta tatu upande wa juu kulia zenye maumbo ya mraba badala ya duara, umbo la picha katika sehemu zenye kona ni tofauti na machapisho kutoka mtandao wa X, muonekano wa picha ya wasifu.

Katika siku za karibuni kumekuwa na uwepo wa picha zenye ujumbe kama huo zikitumia utambulisho wa Rais Samia ili kupotosha uhalisia. Rejea hapa, hapa na hapa. Epuka kusambaza machapisho, picha au video ambazo unapata mashaka kuhusu uhalisia wake kabla ya kuthibitisha ili kuepusha upotoshaji.​
Back
Top Bottom