KWELI Rais Samia amesema tumekopa mkopo huu, lakini mtalipa nyie

KWELI Rais Samia amesema tumekopa mkopo huu, lakini mtalipa nyie

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Kume Kuwepo na video inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, iki ambatana na nukuu inayodai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisema: "Tumekopa mkopo huu, lakini mtalipa nyie.
SAMIA.jpg
 
Tunachokijua
Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wa awamu ya sita,ameshika nafasi hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa Rais Hayati Joseph Pombe Magufuli wa awamu ya tano.

MADAI

Kumekuwepo na video inayosambaa mitandao ya kijamii hususan Facebook ikiambatana na nukuu inayodai kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ‘’Tumekopa mkopo nafuu lakini mtaulipa nyie’’

UHALISIA

Baada ya ufatiliaji wa kidigitali imebainika kuwa madai hayo ni yakweli lakini video hiyo ni ya miaka minne(4) iliyopita, Oktoba 10, 2021 wakati Rais Samia akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya uviko 19.

Alisema maneno hayo baada ya kutoa onyo kwa mawaziri na wakurugenzi wa halmashauri kutumia fedha za miradi katika ujenzi na ununuzi wa vifaa. Hivyo video hiyo ni ya kweli na aliyasema maneno hayo lakini si video ya 2026 kama ilivyosabazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Back
Top Bottom