Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini. Alianza kuwa rais Machi 19, 2021, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais John Magufuli. Kabla ya kuwa rais, Samia alihudumu kama Makamu wa Rais tangu 2015. Pia amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Leo Oktoba 22, 2024 Kumeibuka 'Post' ya Akaunti ya Mtandao wa Kijamii inayotumia jina la
SafariMojanaSamia yanye picha ya Rais Samia iliyowekewa nukuu yenye maneno:
"
Tunataka anayepokea simu naye awe na salio ili kuimarisha uchumi"
Upi uhalisia wa Post na Nukuu hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa nukuu hiyo imetengenezwa na kufanya ionekane kama Post ya ukurasa unaotumia jina la
SafariMojanaSamia lakini nukuu hiyo haikuwahi kuchapishwa na Ukurasa huo.
Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefuatilia Hotuba za Rais Samia za hivi karibuni (Tazama
hapa) lakini hakuna ushahidi ikimuonesha au kusikika akitoa kauli hiyo katika hotuba na wala kuchapisha katika kurasa zake.