SI KWELI Rais Samia amesema wanataka anayepokea simu naye anakatwa salio ili kuimarisha Uchumi

SI KWELI Rais Samia amesema wanataka anayepokea simu naye anakatwa salio ili kuimarisha Uchumi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
si kweli (2)samia.jpg
 
Tunachokijua
Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini. Alianza kuwa rais Machi 19, 2021, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais John Magufuli. Kabla ya kuwa rais, Samia alihudumu kama Makamu wa Rais tangu 2015. Pia amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Leo Oktoba 22, 2024 Kumeibuka 'Post' ya Akaunti ya Mtandao wa Kijamii inayotumia jina la SafariMojanaSamia yanye picha ya Rais Samia iliyowekewa nukuu yenye maneno:

"Tunataka anayepokea simu naye awe na salio ili kuimarisha uchumi"

Upi uhalisia wa Post na Nukuu hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa nukuu hiyo imetengenezwa na kufanya ionekane kama Post ya ukurasa unaotumia jina la SafariMojanaSamia lakini nukuu hiyo haikuwahi kuchapishwa na Ukurasa huo.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefuatilia Hotuba za Rais Samia za hivi karibuni (Tazama hapa) lakini hakuna ushahidi ikimuonesha au kusikika akitoa kauli hiyo katika hotuba na wala kuchapisha katika kurasa zake.
Habari Wanajamvi..

Katika pitapita zangu huko mtandaoni nimekutana na picha hii inayoonesha kama imemnukuu Rais Samia. Je, nukuu hii ina ukweli wowote? Na ni kweli aliyasema wapi haya?

1730468403502.jpeg
 
Nimekutana nayo huko mitandaoni hasa hasa kwenye mtandao wa X. Hivi kuna ukweli ndani yake kuwa Mama Samia amezungumza na TCRA kuwa ili simu iunganishwe kwa mpokeaji, inatakiwa mpigaji simu na mpigiwa wawe na salio ili kuimarisha uchumi?

1730468361328.jpeg
 
Back
Top Bottom