Rais Samia ametenda haki katika uteuzi wa wagombea Ubunge

Afadhali chawa,wewe ni papasi.
 
Bhange haraam
 
 
Ikifika mwaka 2030 Lucas hajapewa hata ukatibu mwenezi msaidizi itashangaza sana
 
Pambana na mapambio huku kitaa pagumu sana!!
 
Kumsifia kiongozi bila kuhoji uhalisia ni sawa na kumpongeza nahodha anayeongoza meli kuelekea kwenye mwamba – kwa sababu tu ana sare nzuri na tabasamu. Taifa linahitaji watu wanaotumia akili, si hisia; hoja, si porojo za kishabiki.

Samia ni Rais, si mungu. Anaweza kusifiwa kwa mazuri yake lakini lazima awajibishwe kwa mapungufu yake. Kumsifu kupita kiasi ni aina ya usaliti wa kimyakimya kwa wanyonge wanaolia hospitalini bila dawa, kwa vijana waliokata tamaa bila ajira, na kwa wapinzani waliodhulumiwa haki zao.

Ushabiki wa kipofu unaua Taifa. Badala ya kupiga makofi kwa kila kitu, jiulize: Je, maisha ya Mtanzania wa kawaida yamebadilika kwa vitendo au kwa hotuba tu? Kama kweli ni ‘nyota ya matumaini’, mbona giza bado linatawala vijijini na mijini?

Simba wa nyika halisi hapishi mafisadi, haogopi ukosoaji, na hasafiri huku nyuma mambo yanawaka moto. Kama wewe ni mfuasi wa kweli, msifie kiongozi wako kwa kuisema kweli – si kwa kumlinda na maneno ya kupendeza lakini yasiyo na maana kwenye maisha ya wananchi.
 
Hivi kweli unaamini hakuna malalamiko, manung’uniko wala lawama? Au unaishi kwenye anga la propaganda za kusifiwa? Tanzania si jumba la maigizo, na si kila mchakato wa kupaka rangi unamaanisha rangi yenyewe ni safi.

Uteuzi wa wagombea haumaanishi haki tu kwa macho ya waliochaguliwa, bali kwa midomo ya waliokatwa bila sababu, waliotelekezwa licha ya uwezo, na waliopitishwa kwa mizengwe ya mapenzi ya “system”. Ukiona watu wamekaa kimya, si kwamba wameridhika — wapo wanaovumilia kwa maumivu, kwa sababu wanajua sauti yao haina pa kupokelewa.

Mchakato wa haki haupimwi kwa sifa za mdomo, bali kwa macho ya wananchi na kwa hofu ya Mungu wa kweli — si Mungu wa kisiasa anayetajwa ili kuficha njama. Mungu halali, na hata ukitumia jina Lake kusafisha uonevu, ukweli utabaki palepale: haki ya kweli haitangazwi, hujionyesha kwa matokeo ya amani ya ndani, si kimya cha huzuni.

Mwisho wa siku, utawala wa kweli haujengwi kwa kusifiwa, bali kwa kukosolewa. Usituambie haki imeonekana kutendeka wakati chaguzi za ndani zimejaa kelele visiwani, mijini na vijijini. Kama kuna ucha Mungu wa kweli, basi na ukweli uwe wazi — hata kama unaumiza masikio ya wapiga tarumbeta wa kusifia bila kuona.
 
Mnachochea Watanzania “watiki” kwa uchaguzi ambao hata kalamu za kuhesabu zimechorwa kabla ya kura kupigwa. Bila reforms, kutiki ni kuhalalisha mzaha wa kidemokrasia unaobebwa na mfumo, si sauti ya wananchi. Tumekataa kuwa sehemu ya maigizo ya CCM.
 
Hii ni kwa watanganyika na sio wazenji.

Kazi ni kipimo cha utu
 
Mcha Mungu anafungia Makanisa ya Ufufuo na Uzima!!!!
 
Acha ujinga wewe chawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…