Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi milioni 100 kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi na Awali inayojengwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika wa Ebeneza, Kanisa Kuu, mkoani Shinyanga.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katambi amesema mchango huo unaakisi dhamira ya Rais Samia ya kuunga mkono juhudi za taasisi za dini katika kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya kujifunzia.
"Rais Samia amenituma kwako Baba Askofu kuchangia fedha ambazo tayari mpaka sasa ninavyosema, alinipa na tumeziingiza kwenye akaunti ya kanisa, shilingi milioni mia moja (100,000,000)"
"Kwa hiyo na hapa mbele yako, na mimi nitoe sadaka ya shukrani kwa haya ambayo umeyafanya, lakini pia kuungwa mkono kwa kanisa na mapenzi mema ambayo mnayafanya. Kwa hiyo Baba Askofu, kwa kuwa ujenzi ni hatua, na mimi naunga mkono hiki Mheshimiwa Rais alichokitoa, naunga mkono kwa kutoa mifuko mia tano (500) ya simenti"
Soma Pia: Kanisa la KKKT Makete lamzawadia Rais Samia Tuzo ya Amani na Umoja
Katika hatua nyingine, Katambi ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa shule hiyo, ambapo jumla ya shilingi milioni 402.39 zimepatikana kupitia michango ya fedha taslimu na ahadi mbalimbali kutoka kwa waumini na wadau waliojitokeza kuchangia mradi huo