Rais Samia ametunyoshea kidole vijana kwa kuwa hatueleweki

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Leo Rais ametunyoshea mkono vijana kwa kuwa hatueleweki. Hatuna mipango. Amesema kuwa Vijana wamekuwa wabeba maono/ Mabegi wa watu. Hatuna dira kama Vijana hata sera ya tangu 2007 haina maboresho yoyote.

Nikiri kuwa Mimi ni sehemu ya tulioshiriki kuandaa rasimu ya Vijana ambayo sasa ni miaka 6 sijaona kinachoendelea. Sijui walikwama wapi.

Mhe Rais anajaribu kutufungua macho na ufahamu, lakini sina uhakika kama Watu wanamuelewa.

Leo sitaki kuongea mengi, ila ninataka kumaliza kwa kusema UVCCM hotuba hii ni yetu hasa viongozi kwa asilimia mia Moja. Nyie ndiye wenye kundi kubwa la Vijana, lakini bado hamjasidia Rais na Serikali katika kupambana na changamoto.

UVCCM bado hatujafanya KAZI ile ambayo mama anaitaka. Tupunguze kusifia Wabunge na Mawaziri. Tufanye KAZI ya kutafuta majibu na majawabu ya changamoto za Vijana na nchi kwa ujumla.
 
Binafsi huyu Mama tangu aingie madarakani ilinichukua muda kumuelewa ila kwa sasa kapandisha graph na nahsi mbeleni atakuwa Raisi bora kuwahi kutokea. Timpe Muda
 
Sijakuelewa hata hii ni hotuba au wewe ndio umeweka maneno yako?
 
Mama alipogusia hamisho la wamachinga huko Moro kapiga punch line moja nikasikia vijana wanaimba tunaimani na Samia! Mi mwenyewe nae Prezdaa wangu! Mama akaze tu watamwelewa Hawa waliovizoea sana viti vyao.
 
Sio kila kijana anafaa kuwa kiongozi, ndio maana kuna vetting rais aitumie vizuri vinginevyo tutapata kina Sabayanga wengi zaidi.
 
Leo Rais ametunyoshea mkono vijana kwa kuwa hatueleweki. Hatuna mipango. Amesema kuwa Vijana wamekuwa wabeba maono/ Mabegi wa watu. Hatuna dira kama Vijana hata sera ya tangu 2007 haina maboresho yoyote.

Nikiri kuwa Mimi ni sehemu ya tulioshiriki kuandaa rasimu ya Vijana ambayo sasa ni miaka 6 sijaona kinachoendelea. Sijui walikwama wapi.

Mhe Rais anajaribu kutufungua macho na ufahamu, lakini sina uhakika kama Watu wanamuelewa.

Leo sitaki kuongea mengi, ila ninataka kumaliza kwa kusema UVCCM hotuba hii ni yetu hasa viongozi kwa asilimia mia Moja. Nyie ndiye wenye kundi kubwa la Vijana, lakini bado hamjasidia Rais na Serikali katika kupambana na changamoto.

UVCCM bado hatujafanya KAZI ile ambayo mama anaitaka. Tupunguze kusifia Wabunge na Mawaziri. Tufanye KAZI ya kutafuta majibu na majawabu ya changamoto za Vijana na nchi kwa ujumla.
Yaani kwa namna ulivyo andika, kama kuna mgeni basi anaweza kudhania kwamba vijana wote ndani ya hii nchi ni uvccm kama wewe! Kumbe mambo ni tofauti kabisa
 
Inabidi tubadilike sasa, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom