Rais Samia amewasha moto wa Maendeleo usiozimika

Rais Samia amewasha moto wa Maendeleo usiozimika

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu watanzania

Rais Samia Amewasha moto wa Maendeleo Usiozimika, Ni Moto katika Elimu, Afya, Miundombinu, huduma za maji Safi na salama, umeme mpaka vijijini, Moto katika miradi ya kimkakati, Moto katika utalii, uwekezaji na Biashara, Amewasha Moto katika kilimo.

Ni Moto uwakao pasipo kuzima, Ni Moto unaoteketeza wazembe na wabadhilifu wa Mali za umma, Ni Moto kwa wavivu, Ni Moto katika kila kichaka kilicho kikwazo katika kuwahudumia watanzania.

Ni Moto wa matumaini katika mioyo ya watanzania,Ni Moto unao iheshimsha Tanzania,Ni Moto unao angaza penye giza, Nchi yote Ni mwanga na Nuru kutokana na Moto alio uwasha Rais Samia,Ni Moto unaoacha majeraha na majuto kwa wenye kugusa pesa za umma,Ni Moto unaoacha vicheko kwa wanyonge,Ni Moto unaoleta Tabasamu kwa walio kuwa gizani,Ni Moto unaowaangazia wavuvi Ziwani na mitoni,Ni Moto unaoleta hamasa ya kulima kwa wakulima.

Ni Moto usioluka Kaya ya mtanzania yeyote,Ni Moto wa kazi ,Ni Moto wa matumaini,Ni Moto wa kusonga mbele kwa kujiamini na Tabasamu,Ni Moto wa kuondoa hofu mioyoni mwa watanzania,Ni Moto wa kuwaunganisha watanzania,Ni Moto unaowafanya watanzania wazungumze lugha moja.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Naomba uongozi wa humu kuniunganishia Uzi huu na huo mwingine ambao haujakamilika
 
Back
Top Bottom