Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na Fadhili kwa kumsafirisha na kumfikisha Salama Nchini Ufaransa Rais Wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge.
Ambapo katika mkutano huo Rais wetu ataongoza kama Mwenyekiti Mwenza ,heshima ambayo Tanzania tumepewa kutokana na kutambua mchango mkubwa na juhudi za kipekee za Rais wetu mpendwa katika kuhakikisha kuwa Dunia inajielekeza katika matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa .
Ambayo yamekuwa na athari kubwa kiafya na kusababisha vifo kila mwaka hususani kwa wanawake ambao wamekuwa wahanga na waathirika wakubwa sana wa athari zitokanazo na matumizi ya kuni na mkaa. Rais wetu mpendwa kama Mama na anayetambua athari hizo amekuwa msitari wa mbele kabisa kuiamsha Dunia na kumuokoa Mwanamke na athari hizo.
Kwa kuyataka mataifa yaliyoendelea na taasisi za kifedha kutoa fedha za kutosha katika kufanikisha na kuwekeza katika suala la matumizi ya nishati safi ya kupikia,pamoja na kutunga sera na sheria zitakazo chochea matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Tuendelee kumuombea afya njema Rais wetu wakati wote atakapokuwa huko mkutanoni. Mkono na uso wa Mungu uwe pamoja naye na aendelee kumpatia kibali na Neema wakati wote.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.