Rais Samia amewatuma Mabalozi wakaulize wenzetu wamefanya uchawi gani kukua haraka kiuchumi

Rais hujui nini cha kufanya ili tuendelee?! Unataka kukopi historia ya nchi nyingine?! Duh!
 
Vile vile mama aambiwe kuwa hizo nchi hazikuingia mikataba mibovu kama huu wa bandari.
 
Mkuu naona haufikirii kwa usahihi.
- kwamba katiba imetukatili kwa kumuweka madarakani mtu asiyejuwa kwanini nchi kama thailand imetuacha kimaendeleo.
-Sasa hebu uniambie katiba inatuhakikishiaje kuwa mtu anayekwenda ikuru kwa njia ya kura anafahamu chanzo cha udumavu wetu?

- Kama katiba inatuhakikishia kuwa atakeye kaa kwenye kitu cha urais atakuwa anafahamu chanzo cha udumavu wetu(kwani alipigiwa kura tofauti na Samia kwenda ikuru), kwanini tumedumaa? Au takwa la katiba kwa rais ni kujuwa tu chanzo cha tatizo na si kuchukuwa hatuwa dhidi ya tatizo?

-alafu,.........
 
Siri kubwa ya Asia, Singapore kwa mfano.
- Wanachagua na kuteua bright minds kuwa katika majukumu serikalini na hata mawaziri. hakuna nepotism ya kuteua mtu kwa sababu baba yake alikuwa kiongozi ktk chama.

-Hawacheki kuhusu ufisadi na hawaangalii sura. Ingekuwa nchi za Asia, mikataba ya ajabu ajabu tangu ianze kusainiwa hapa tz, wengi wangeshakula vitanzi. Hata huu wa bandari kuna watu wangeshakuwa buriani.
 
Tatizo ni wizi wa viongozi kuuza rasilimali za inchi,kupeana vyeo kindugu bila kuzingatia uwezo wa mtu,rushwa, kutokuwa na uzarendo hasa kwa viongozi, na CCM yenyewe imechoka
 
Tanzania haitakaa iendelee kuvuka ngazi ya LDC hadi itakapopata UONGOZI BORA.

Nyerere mwenyewe alitaja kwa usahihi kabisa nguzo kuu tatu za msingi wa maendeleo: watu, siasa safi na uongozi bora. WATU tupo naturally. Mwenyenzi Mungu katuweka kwenye nchi yenye baraka zote.

Kwa bahati mbaya sana JKN mwenyewe akaanza kuongoza nchi kwa misingi ya SIASA DHAIFU na UONGOZI WA MTU MMOJA (one man show). Uongozi wake ulikuwa bora kwa vile yeye binafsi alikuwa na maadili ya kipekee. Hadi anaondoka msingi mbovu wa siasa na uongozi (mfumo CCM) ulibaki na kudumu vile vile hadi leo huku mafisadi wa kila aina wakiingia madarakani.

In short, TUSAHAU KABISA habari ya maendeleo kwa aina ya siasa na mfumo wa uongozi tulio nao. Sina jibu nisije kuunganishwa kwenye kadhia inayoendelea.
 
Muandishi wewe umetafsiri vibaya.

Rais kusema uchawi gani , Amemaanisha mbinu gani hajamaanisha matunguli
...Ina maana hajui Mbinu zilizotumika kuzifanya Nchi zilizotajwa Zirndelee ! Hata MBINU hajui Mpaka Watu anaoteua wakaulize ???
 
Kama anafanya akiwa na dhamira ya haki na Sheria za haki hakuna tatizo.
...Kuzimilikisha Bandari zetu zote Kwa Mkataba usiojulikana Wazi ni WA Muda gani, ndio kuwa na Dhamira ya Haki ???
Pleeaaseee...![emoji35]
 
Ila kiukweli HATERS NA NYUMBU mnatia huruma wakati mwingine; yaani mnataka kusema mmeshindwa kuelewa mantiki ya alichokisema hapo au mnajitoa ufahamu tu in the name of hatred?!!!!

Hamuwezi kumshinda kwa viroja vyenu vya kijingajinga kama hivi nyie kenge. Mabalozi wanalazimika kuwa na jicho la 'wizi' wa kiuchumi na sio kwenda kula bata tu na kusinzia.......simple tu kuelewa ukiwa katika akili huru.

Mama ataendelea kupiga hatua za kimaendeleo mpende msipende.
 
ikumbukwe huyo ni form four failure na alikwenda kuolewa baada ya kumaliza form four.

Elimu yake mpaka alipofika ni ya kuunga unga
 
Thailand wameendelea kwa sababu ya uwekezaji wenye tija ambao uko wazi kwa wananchi.Huko hakuna upuuzi wa kuuza Maliasili kama huu upuuzi wa uuzaji maliasili Tanganyika ikiwemo bandari.Kama kweli rais hajui wenzetu wamefanyaje hadi kufika hapo walipo kimaendeleo basi aachie hiyo nafasi.
 
Hili ndiyo tatizo kuu imagine dhahabu iliyochimbwa Geita na Kahama kama 50% tu ya kilichovunwa tangu 98 walipoanza kuzalisha kingetumika kuleta maendeleo kanda ya ziwa ingekuwa na maendeleo makubwa sana lakini leo hii hata jirani na mgodi kuna shule hazina matundu ya vyoo achilia mbali madarasa.
 
Wana jamvi samahani ....naomba kuuliza ili uwe PRESIDENT ni sifa zipi muhimu lazma uwe nazo ....... nahisi kuna mahali tulisha feli kama taifa
 
Kama kweli huyo bibi kasema hivyo, bac uwezo wake wa akili una walakini.
 
Tanzania na imani za kishirikina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…