Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza na Balozi wa Shina Namba 1, katika Kata ya Komunyika, Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, Ndugu Juma Ahmed Rugina na kumpongeza kwa kuongoza shina hilo kwa miaka ishirini.
Balozi Mzee Rugina amezungumza na Rais Samia kupitia simu ya mkononi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Ndugu Daniel Chongolo ambaye ametembelea shina hilo la kukagua uhai na uimara wa chama kwenye ngazi ya mashina na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.
Katika mazungumzo hayo, Balozi Rugina amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kufungua fursa za maendeleo kwa wananchi wa Kasulu na mkoa mzima wa Kigoma kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya na elimu ambapo amesema miaka ya nyuma wakati kama huu mifugo yao na vitu vingine vilikuwa vinauzwa kwa ajili ya michango, kuchangia ujenzi wa madarasa ya shule.
Aidha, Balozi Rugina amemuomba Rais Samia kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa karavati mtaani hapo pamoja na kadi za uanachama kwa wakereketwa wote wa CCM wa shina hilo pamoja na mashina mengine wilayani Kasulu na Mkoa wa Kigoma ambapo katika shina hilo kuna wanachama 64 na wakereketwa wengi wasio na kadi.
Katika hatua nyingine Rais Samia alimuomba balozi huyo kuwahamasisha wanachama wake na wananchi kwa ujumla, kushiriki kwenye mambo ya maendeleo kikamilifu ikiwemo kuhakikisha wanachanjwa chanjo ya kujikinga dhidi ya Uviko 19.
Chongolo pia, ametembela na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa Chuo cha Veta Kasulu, na ujenzi wa Shule ya Sekondari Mayonga.
Chongolo pamoja na sekretarieti ya Halmashauri kuu ya chama hicho, wapo Kigoma kwa ziara ya siku mbili kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuhamasisha uhai wa mashina wa chama hicho.