JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Nukuu ya Rais Samia Suluhu Hassan alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa jingo la benki, Machi 5, 2022 amemtaja staa mkongwe wa Bongo Fleva kwa kunukuu moja ya mstari wake aliowahi kuuimba kwenye kazi zake za muziki.
Hii hapa nukuu ya mama Samia:
"Mwanangu Juma Nature alisema, kwani wao waweze wana nini hata sisi tushindwe tuna nini?" amesema Rais Samia wakati akihimiza benki za Tanzania kwenda kuwekeza nje ya nchi kama ambavyo benki za nje zinavyokuja kuwekeza Tanzania.
Juma Kassim 'Nature' au Juma Nature ni msanii ambaye miaka 10 hadi 15 nyuma alikuwa ndiye 'Diamond' wa kipindi hicho, alifanya kazi nyingi zilizotikisa nchi, alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanzakwanza wa muziki huo wa kizazi kipya kupata tuzo kutoka nje ya Tanzania.
Makazi yake yakiwa Temeke huku kazi nyingi akifanya na Prodyuza P Funk alijulikana kwa misemo yake hasa ya mtaani, alikuwa na uwezo wa kurap na kuimba pia.
Kwa miaka ya hivi karibuni amepoteza nguvu ya umaarufu wake katika muziki japokuwa amekuwa akiendelea kufanya kwa kutoa nyimbo kadhaa lakini hazijapata 'airtime' kama ilivyokuwa zamani.