Rais Samia ampa Mzee Zahir Zorro Tsh. Milioni 10

Rais Samia ampa Mzee Zahir Zorro Tsh. Milioni 10

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) amemtembelea na kumjulia hali Mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa dansi Zahir Ally Zorro nyumbani kwake Kigamboni Jijini Dar es salaam kwa lengo la kumpa pole kutokana na changamoto za kiafya anazopitia.

1773050992461.png

Katika ziara hiyo, Hamis Mwinjuma amemkabidhi Zahir Ally Zorro kiasi cha shilingi milioni 10 taslimu kama salamu za pole na faraja kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan, huku akimtakia kupona haraka na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Soma > Mwana FA ampa vifaa vya mazoezi Mzee Zahir Ally Zorro

Akizungumza baada ya kumtembelea Mkongwe huyo, Naibu Waziri Mwinjuma amesema Serikali inaendelea kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na Wasanii Wakongwe katika kukuza na kuendeleza sanaa na utamaduni wa Tanzania, na kuongeza kuwa Wakongwe hao ni hazina muhimu ya Taifa na wanastahili kuenziwa pamoja na kupewa faraja wanapokumbwa na changamoto mbalimbali za kiafya au kijamii.

 
Wanachezea hela zetu bure,kuna wapigania uhuru wengi wanaumwa na wamezeeka zaidi ya huyo zahir wanapewa 35000 ya tasaf...
Matumizi mabaya ya fedha za umma
 
Dah huyu Mzee anasumbuliwa na nini?

ova
 
Back
Top Bottom