Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

Anna Nkya

Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
69
Reaction score
341
Jana nilisambaa video ikimuonesha Spika Job Ndugai akitoa kauli zilizofanya watu wahoji nia yake dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Katijka hali ya kushangaza, Spika Ndugai ambaye alikuwa mmoja wa wapiga zumari wakubwa wa Serikali iliyopita, alionekana kukandia mikopo inayokopwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Mfano akizungumzia mkopo wa Trilioni 1.3 ambao Serikali imekopa kutoka IMF, Ndugai amesema ni "Mikopo mikubwa mikubwa isiyoeleweka". Ndugai alishangaa kitendo cha Serikali "KUPIGA MAKOFI" baada ya kupokea mikopo hiyo, akisema kwamba mwaka 2025 watu wataamua kama watapenda kuwa na Serikali inayokopa kopa.

RAIS SAMIA 'AMPIGA"

Akihutubia baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa SGR kipande cha Makutopora hadi Tabora , Rais Samia amesema kuna jitihada kubwa za kumvunja moyo katika mikopo, na akatoa hoja za kueleweka kueleza kwa nini tunakopa.

Rais amesema lazima tuendelee kukopa kwa sababu:

1. Tuna miradi ya matrilioni ambayo ilishaazishwa na lazima tuitekeleze kwa wakati. Alitolea mfano wa SGR kwamba ni uwekezaji wa trilioni zaidi ya 14, hivyo hatuwezi kusubiri ni lazima tukope kutekeleza.

2. Mikopo inayotolewa ni mikopo nafuu. Hili linaijibu hoja ya Ndugai aliyejaribu kuonesha kwamba deni la Taifa halistahimiliki akitia chumvi kwamba ipo siku "NCHI ITAPIGWA MNADA". Rais Samia amesema tunatafuta mikopo nafuu akisema kubwa ni uwezo wa kushawishi

3. Kukopa ni kawaida. Tanzania inakopa tangu enzi na enzi, Marais wote walikopa huku Rais aliyepita (Magufuli) akikopa zaidi kwa kuangalia kipindi alichokaa madarakani (Ndugai alikuwa anashangilia tu).

VIDEO (kwa hisani ya @mamayukokazini) HIYO HAPO CHINI
 
aika manka ndede
 
Mama tunakuaminia piga kazi hizo porojo zione za kawaida usirudi nyuma.
 
Magufuli alikopa zaidi ya trillion 30 peke yake ndani ya miaka 5 tu, lakin Huyo Ndugai hakuongea kitu. Lakin huyu mama amekopa trillion 1.3 Ndugai anapiga kelele kila mahali!
Bi Mkubwa amekopa TRILIONI 7.7 within 4 months. It's means akikaa hadi 2025 atakuwa amekopa almost TRILIONI 100.
 
Kupata mkopo ni uwezo wa 'ushawishi'. Huo uwezo wa kushawishi ni wa namna gani, wajuzi wa mambo tueleweshen hapo. maana ushawishi unaweza kuwa: nipe mkopo alafu nitakuachia bandari ya dasilam kwa miaka 20!
 
Back
Top Bottom