Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

Magufuli alikopa zaidi ya trillion 30 peke yake ndani ya miaka 5 tu, lakin Huyo Ndugai hakuongea kitu. Lakin huyu mama amekopa trillion 1.3 Ndugai anapiga kelele kila mahali!
Naona kama vile siku hizi Ndugai NAE anajipima ubavu na Mtemi Hangaya.
 
Wewe wasema.. mikataba imeisha sainiwa na watu wapo site. Kwanini isiishe?
Pole sana,
walewale waliokuwa wanajilia mihela awamu ya giza wapo na wanaendelea na ulaji. Uzuri wake mtakuja washangilia kwa kufanikiwa kutokubakisha mihela. Mambo ni yaleyale, vilevile kwani chama ni kilekile.
 
Samia leta umeme, achana na kesi za kina mbowe, sapoti mchakato wa katiba, hakikisha pesa inapatikan mtaani halafu sikiliza nchi itakavyosimama na wewe.
 
Aliyeleta wazo la ujenzi wa sgr sijui alifikiria nini. Kitu imekula pesa na hamna tulichofanikiwa hadi sahivi.
 
Magufuli alikopa zaidi ya trillion 30 peke yake ndani ya miaka 5 tu, lakin Huyo Ndugai hakuongea kitu. Lakin huyu mama amekopa trillion 1.3 Ndugai anapiga kelele kila mahali!
Mikopo ya Magufuli ilielekezwa kwenye miradi ya maendeleo Kama barabara, umeme, reli na maji. Ni miradi ambayo inazalisha au inachochea uchumi.

Mkopo wa covid 19 umeelekezwa kwenye miradi ya huduma kwa jamii (ujenzi wa madarasa, kutoa elimu ya chanjo/ kununua chanjo), ni miradi ambayo haizalishi. Kwa hiyo kwa mkopo huo wa covid 19 ni mzigo kwa Taifa.

JPM aliona mbali akaukataa kwa sababu Kama wana nia ya kutusaidia na janga la covid wangetupa grant au kutupunguzia madeni siyo kutuongezea mzigo wa Deni ambalo halina impact ktk kukuza uchumi wetu.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Kupata mkopo ni uwezo wa 'ushawishi'. Huo uwezo wa kushawishi ni wa namna gani, wajuzi wa mambo tueleweshen hapo. maana ushawishi unaweza kuwa: nipe mkopo alafu nitakuachia bandari ya dasilam kwa miaka 20!
Nadhani alimaanisha ^uwezo wa kukubali kushawishiwa^
 
Aliyeleta wazo la ujenzi wa sgr sijui alifikiria nini. Kitu imekula pesa na hamna tulichofanikiwa hadi sahivi.

Hizo ni sababu shutumizi. SGR ingeenda spidi iliyopangwa, sasa hivyo ingekuwa ndiyo chanzo cha mapato ya kujengea miradi mingine.

#^Car-taaWar-who-knee^
 
Wewe wasema.. mikataba imeisha sainiwa na watu wapo site. Kwanini isiishe?
Wapo saiti wanatumbua hela na kuzuga as though wanafanya kitu cha maana. Ndiyo maana barabara ya lami, kilometa moja wanajenga kwa zaidi ya miezi ^sea-tar^ na nusu.
 
Jana nilisambaa video ikimuonesha Spika Job Ndugai akitoa kauli zilizofanya watu wahoji nia yake dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Katijka hali ya kushangaza, Spika Ndugai ambaye alikuwa mmoja wa wapiga zumari wakubwa wa Serikali iliyopita, alionekana kukandia mikopo inayokopwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Mfano akizungumzia mkopo wa Trilioni 1.3 ambao Serikali imekopa kutoka IMF, Ndugai amesema ni "Mikopo mikubwa mikubwa isiyoeleweka". Ndugai alishangaa kitendo cha Serikali "KUPIGA MAKOFI" baada ya kupokea mikopo hiyo, akisema kwamba mwaka 2025 watu wataamua kama watapenda kuwa na Serikali inayokopa kopa.

RAIS SAMIA 'AMPIGA"

Akihutubia baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa SGR kipande cha Makutopora hadi Tabora , Rais Samia amesema kuna jitihada kubwa za kumvunja moyo katika mikopo, na akatoa hoja za kueleweka kueleza kwa nini tunakopa.

Rais amesema lazima tuendelee kukopa kwa sababu:

1. Tuna miradi ya matrilioni ambayo ilishaazishwa na lazima tuitekeleze kwa wakati. Alitolea mfano wa SGR kwamba ni uwekezaji wa trilioni zaidi ya 14, hivyo hatuwezi kusubiri ni lazima tukope kutekeleza.

2. Mikopo inayotolewa ni mikopo nafuu. Hili linaijibu hoja ya Ndugai aliyejaribu kuonesha kwamba deni la Taifa halistahimiliki akitia chumvi kwamba ipo siku "NCHI ITAPIGWA MNADA". Rais Samia amesema tunatafuta mikopo nafuu akisema kubwa ni uwezo wa kushawishi

3. Kukopa ni kawaida. Tanzania inakopa tangu enzi na enzi, Marais wote walikopa huku Rais aliyepita (Magufuli) akikopa zaidi kwa kuangalia kipindi alichokaa madarakani (Ndugai alikuwa anashangilia tu).

VIDEO (kwa hisani ya @mamayukokazini) HIYO HAPO CHINI
Swali la kujiuliza. Hii miradi imeanza kipindi hiki alipokabidhiwa madaraka au enzi ya JPM ambayo ilikuwa inaenda kasi kuliko hata sasa nayeye akiwepo.
Kwani Hayati alikuwa anapata wapi fedha??
Tunakopa jumlisha Tozo na bado wanazipiga ile mbaya.
Waziri wa fedha akiongoza jopo.
Kuna siku taifa litajutia haya.
Tuna rasilimali lukuki hakuna usimamizi. Tunakimbilia kukopa.

Katiba Katiba na Tume huru.
Pole pole uko wapi.

Ugaidi ni siasa uchwara.
Hakuna Gaidi Tanzania!
 
Viongozi vipofu, wasio maono huliingiza taifa hili kwenye mitihani mikubwa.
 
Back
Top Bottom