Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

Rais Samia 'ampiga' Spika Ndugai

Ndugai ni mnafiki wa kutupa.

Si ajabu akajitokeza kesho kutwa kujibaraguza kama alivyofanya awamu iliyopita baada ya kujibiwa kuhusu bandari ya Bagamoyo.
 
Mikopo ya Magufuli ilielekezwa kwenye miradi ya maendeleo Kama barabara, umeme, reli na maji. Ni miradi ambayo inazalisha au inachochea uchumi.

Mkopo wa covid 19 umeelekezwa kwenye miradi ya huduma kwa jamii (ujenzi wa madarasa, kutoa elimu ya chanjo/ kununua chanjo), ni miradi ambayo haizalishi. Kwa hiyo kwa mkopo huo wa covid 19 ni mzigo kwa Taifa.

JPM aliona mbali akaukataa kwa sababu Kama wana nia ya kutusaidia na janga la covid wangetupa grant au kutupunguzia madeni siyo kutuongezea mzigo wa Deni ambalo halina impact ktk kukuza uchumi wetu.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Amemaliza miradi gani kati ya hiyo baada ya kukopa trillion 30 na amehangaika ndani ya miaka 5 akidanganya madunya kama wewe kuwa tunajenga fedha za ndani
 
Majungu tu..

Hii nchi imekuwa na viongozi wa hovyo sana
 
CCM Ni kituko
Ndugai ameunga mkono Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo anaitwa Msaliti wa Serikali ya Awamu ya 5 kigeugeu
Ndugai katoa matamko wa Mkopo kapewa jina lingine Mtu aliyekuwa anaunga mkono Serikali ya Awamu 5 wapiga zumari wakubwa Serikali ya Awamu 5

Tuelewe nini
Unashangaa nini sasa wakati Ndugai alishasema ana cheti cha mirembe
 
Amemaliza miradi gani kati ya hiyo baada ya kukopa trillion 30 na amehangaika ndani ya miaka 5 akidanganya madunya kama wewe kuwa tunajenga fedha za ndani
Kuna miradi ya muda mfupi kama flyover ya ubungo, Salendar bridge, upanuzi barabara kimara to kibaha, n.k. lakini miradi Kama Sgr na Bwawa la umeme Rufiji ni miradi ya muda mrefu isingeweza kuisha ndani ya miaka mitano.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Jana nilisambaa video ikimuonesha Spika Job Ndugai akitoa kauli zilizofanya watu wahoji nia yake dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Katijka hali ya kushangaza, Spika Ndugai ambaye alikuwa mmoja wa wapiga zumari wakubwa wa Serikali iliyopita, alionekana kukandia mikopo inayokopwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Mfano akizungumzia mkopo wa Trilioni 1.3 ambao Serikali imekopa kutoka IMF, Ndugai amesema ni "Mikopo mikubwa mikubwa isiyoeleweka". Ndugai alishangaa kitendo cha Serikali "KUPIGA MAKOFI" baada ya kupokea mikopo hiyo, akisema kwamba mwaka 2025 watu wataamua kama watapenda kuwa na Serikali inayokopa kopa.

RAIS SAMIA 'AMPIGA"

Akihutubia baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa SGR kipande cha Makutopora hadi Tabora , Rais Samia amesema kuna jitihada kubwa za kumvunja moyo katika mikopo, na akatoa hoja za kueleweka kueleza kwa nini tunakopa.

Rais amesema lazima tuendelee kukopa kwa sababu:

1. Tuna miradi ya matrilioni ambayo ilishaazishwa na lazima tuitekeleze kwa wakati. Alitolea mfano wa SGR kwamba ni uwekezaji wa trilioni zaidi ya 14, hivyo hatuwezi kusubiri ni lazima tukope kutekeleza.

2. Mikopo inayotolewa ni mikopo nafuu. Hili linaijibu hoja ya Ndugai aliyejaribu kuonesha kwamba deni la Taifa halistahimiliki akitia chumvi kwamba ipo siku "NCHI ITAPIGWA MNADA". Rais Samia amesema tunatafuta mikopo nafuu akisema kubwa ni uwezo wa kushawishi

3. Kukopa ni kawaida. Tanzania inakopa tangu enzi na enzi, Marais wote walikopa huku Rais aliyepita (Magufuli) akikopa zaidi kwa kuangalia kipindi alichokaa madarakani (Ndugai alikuwa anashangilia tu).

VIDEO (kwa hisani ya @mamayukokazini) HIYO HAPO CHINI
Kwenye item 2 hapo umesema Ndugai ametia chumvi lakini na wewe umetia chumvi kwenye item 3 hapo kwa kumuwekea mama mdomoni mwake maneno yako haya "Rais aliyepita (Magufuli) akikopa kwa kuangalia kipindi alichokaa madarakani (Ndugai alikuwa anashangilia tu)"

Clip inakusuta kwa sababu nimeisikiliza mwanzo mwisho hakuna sehemu mama amemtaja mtu kwa jina wala kumrejelea directly kwa kauli zake.

Aidha, ungeendelea mbele kwa kumtia mama moyo kwamba hakuna rais ambaye hajawahi kuvunjwa moyo, Magufuli anaendelea kuvunjwa moyo hadi kaburini.

NB.
Alichotakiwa kufanya Mhe. Ndugai ni kupinga ilani ya chama wakati inaandaliwa kwamba italiingiza taifa kwenye madeni ya kuweza kuifanya ikanadiwa, kama chama kisingemsikiliza basi angeibana serikali Bungeni akipinga miradi hiyo ya thamani kubwa kuliko uwezo wa nchi, sasa mama afanyeje leo ambapo miradi iko kwenye ujenzi? Job ana washauri wote wa kisekta walitakiwa wawe wanamuandaa Spika vizuri katika kila anachokifanya na kukisema.

Ila Nkya hoja ya msingi unayo na naikubali na kukukubali pia kwa ujasiri kama wa Askari wa msitari wa mbele. Keep it up!
 
Bi Mkubwa amekopa TRILIONI 7.7 within 4 months. It's means akikaa hadi 2025 atakuwa amekopa almost TRILIONI 100.
Alichotakiwa kufanya Mhe. Ndugai ni kupinga ilani ya chama wakati inaandaliwa kwamba italiingiza taifa kwenye madeni ya kuweza kuifanya ikanadiwa, kama chama kisingemsikiliza basi angeibana serikali Bungeni akipinga miradi hiyo ya thamani kubwa kuliko uwezo wa nchi, sasa mama afanyeje leo ambapo miradi iko kwenye ujenzi? Job ana washauri wote wa kisekta walitakiwa wawe wanamuandaa Spika vizuri katika kila anachokifanya na kukisema. Ukim-fire Job fire na washauri wake.
 
Mama asisubili huyo mgogo aende milembe mwenyewe ampeleke!
Jana nilisambaa video ikimuonesha Spika Job Ndugai akitoa kauli zilizofanya watu wahoji nia yake dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Katijka hali ya kushangaza, Spika Ndugai ambaye alikuwa mmoja wa wapiga zumari wakubwa wa Serikali iliyopita, alionekana kukandia mikopo inayokopwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Mfano akizungumzia mkopo wa Trilioni 1.3 ambao Serikali imekopa kutoka IMF, Ndugai amesema ni "Mikopo mikubwa mikubwa isiyoeleweka". Ndugai alishangaa kitendo cha Serikali "KUPIGA MAKOFI" baada ya kupokea mikopo hiyo, akisema kwamba mwaka 2025 watu wataamua kama watapenda kuwa na Serikali inayokopa kopa.

RAIS SAMIA 'AMPIGA"

Akihutubia baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa SGR kipande cha Makutopora hadi Tabora , Rais Samia amesema kuna jitihada kubwa za kumvunja moyo katika mikopo, na akatoa hoja za kueleweka kueleza kwa nini tunakopa.

Rais amesema lazima tuendelee kukopa kwa sababu:

1. Tuna miradi ya matrilioni ambayo ilishaazishwa na lazima tuitekeleze kwa wakati. Alitolea mfano wa SGR kwamba ni uwekezaji wa trilioni zaidi ya 14, hivyo hatuwezi kusubiri ni lazima tukope kutekeleza.

2. Mikopo inayotolewa ni mikopo nafuu. Hili linaijibu hoja ya Ndugai aliyejaribu kuonesha kwamba deni la Taifa halistahimiliki akitia chumvi kwamba ipo siku "NCHI ITAPIGWA MNADA". Rais Samia amesema tunatafuta mikopo nafuu akisema kubwa ni uwezo wa kushawishi

3. Kukopa ni kawaida. Tanzania inakopa tangu enzi na enzi, Marais wote walikopa huku Rais aliyepita (Magufuli) akikopa zaidi kwa kuangalia kipindi alichokaa madarakani (Ndugai alikuwa anashangilia tu).

VIDEO (kwa hisani ya @mamayukokazini) HIYO HAPO CHINI
 
Magufuli alikopa zaidi ya trillion 30 peke yake ndani ya miaka 5 tu, lakin Huyo Ndugai hakuongea kitu. Lakin huyu mama amekopa trillion 1.3 Ndugai anapiga kelele kila mahali!
Huwezi kopa kwa ajili ya C 19, kopa kwa uwekezaji wa maaana,
Hata ukikopa tr200 kwa miradi itakayorudisha pesa ni sawa!
Pia na usimamizi wa hizo hela, huyu analalamika tu
 
Jana nilisambaa video ikimuonesha Spika Job Ndugai akitoa kauli zilizofanya watu wahoji nia yake dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.

Katijka hali ya kushangaza, Spika Ndugai ambaye alikuwa mmoja wa wapiga zumari wakubwa wa Serikali iliyopita, alionekana kukandia mikopo inayokopwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo ya watu. Mfano akizungumzia mkopo wa Trilioni 1.3 ambao Serikali imekopa kutoka IMF, Ndugai amesema ni "Mikopo mikubwa mikubwa isiyoeleweka". Ndugai alishangaa kitendo cha Serikali "KUPIGA MAKOFI" baada ya kupokea mikopo hiyo, akisema kwamba mwaka 2025 watu wataamua kama watapenda kuwa na Serikali inayokopa kopa.

RAIS SAMIA 'AMPIGA"

Akihutubia baada ya kushuhudia utiwaji saini wa mkataba wa ujenzi wa SGR kipande cha Makutopora hadi Tabora , Rais Samia amesema kuna jitihada kubwa za kumvunja moyo katika mikopo, na akatoa hoja za kueleweka kueleza kwa nini tunakopa.

Rais amesema lazima tuendelee kukopa kwa sababu:

1. Tuna miradi ya matrilioni ambayo ilishaazishwa na lazima tuitekeleze kwa wakati. Alitolea mfano wa SGR kwamba ni uwekezaji wa trilioni zaidi ya 14, hivyo hatuwezi kusubiri ni lazima tukope kutekeleza.

2. Mikopo inayotolewa ni mikopo nafuu. Hili linaijibu hoja ya Ndugai aliyejaribu kuonesha kwamba deni la Taifa halistahimiliki akitia chumvi kwamba ipo siku "NCHI ITAPIGWA MNADA". Rais Samia amesema tunatafuta mikopo nafuu akisema kubwa ni uwezo wa kushawishi

3. Kukopa ni kawaida. Tanzania inakopa tangu enzi na enzi, Marais wote walikopa huku Rais aliyepita (Magufuli) akikopa zaidi kwa kuangalia kipindi alichokaa madarakani (Ndugai alikuwa anashangilia tu).

VIDEO (kwa hisani ya @mamayukokazini) HIYO HAPO CHINI
 
Basi tozo itolewe!! si imefeli,Hadi wameamua ss tukopage Hadi tumalize miradi yetu!?, au hii tozo iliwekwa kwa dhumuni lipi labda!!
 
View attachment 2060580
Why Ndugai?
 
Balile, Ndugai, Luoga, World Bank, Mwigulu, Lipumba, Lissu, Zitto, Mbatia, Mama..... who is who?
 
Back
Top Bottom